Mkutano wa 21 wa Baraza la
Mawaziri la Kisekta
(BLM) la Afya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
katika ngazi
ya Makatibu Wakuu unafanyika leo
tarehe 9 Desemba 2021katika Hotel Verde mjini
Zanzibar.
Mkutano huu na mkutano wa ngazi
ya Maafisa
Waandamizi ambao ulifanyika tarehe 6 hadi 8
Desemba 2021 ni sehemu
ya mikutano ya awali
yenge jukukumu la kupitia na kuwasilisha agenda
na
mapendekezo ya masuala ya afya ya kikanda
yatakayowasilishwa katika Mkutano wa 21
wa
Baraza la Mawaziri la Kisekta la Afya wa Jumuiya
ya Afrika Mashariki
utakaofanyika tarehe 10
Desemba 2021.
Ujumbe wa Tanzania katika
mkutano huu
unaongozwa na Dkt. Fatma H. Mrisho, Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
Viongozi wengine walioambatana naye ni pamoja na Dkt. Othman Mohamed Ahmed, Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia – Tanzania Bara, Bw. Eliabi Chodota, Mkurugenzi Idara ya Miundombinu ya Uchumi na Huduma za Jamii katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Dkt. Abdul S. Ali, Mganga Mkuu na Mkurugenzi Mkuu wa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee, Jinsia na Watoto wa
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Mkutano huu unafanyika mjini
Zanzibar kwa lengo la kuendeleza jitihada za jumuiya katika kutangaza maeneo ya utalii
ndani ya jumuiya. Vilevile kuvutia wageni na kuhamasisha utalii wa ndani kama ilivyosisitizwa katika maonesho ya Utalii ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC-Tourism Expo) yaliyofanyika mapema mwezi Oktoba 2021 Jijini Arusha.
==============================
Ujumbe wa Tanzania |
Ujumbe wa Tanzania |
Ujumbe wa Tanzania |
Sehemu nyingine ya Ujumbe wa Tanzania |
Ujumbe kutoka Kenya |
Ujumbe kutoka Uganda |
Ujumbe kutoka Burundi |