NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Mwita Waitara, akizungumza na Wakuu wa Taasisi na Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, (hawapo pichani), wakati wa kikao kazi kilichofanyika leo Desemba 8,2021 jijini Dodoma.
Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS),Mhandisi Salome Kadunda akitoa taarifa ya Utekelezaji wa wakala huo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Mwita Waitara (hayupo pichani), katika kikao kazi kilichofanyika leo Desemba 8,2021 jijini Dodoma.
Meneja wa Wakala wa Majengo (TBA) Mkoa wa Dodoma,Victor Balthazar,akitoa taarifa ya Utekelezaji wa wakala huo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Mwita Waitara (hayupo pichani), katika kikao kazi kilichofanyika leo Desemba 8,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya Mameneja,Wakuu wa Taasisi na Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Mwita Waitara( hayupo pichani),wakati wa kikao kazi kilichofanyika Desemba 8,2021 jijini Dodoma.
……………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
NAIBU Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Mwita Waitara ameitaka Mamlaka ya Huduma za Usafiri Ardhini(LATRA), kuhakikisha inashughuliki malalamiko ya wadau ikiwemo Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania(TABOA).
Kauli hiyo ameitoa leo Desemba 8,2021 wakati akizungumza na Wakuu wa Taasisi na Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi katika kikao kazi kilichofanyika jijini Dodoma.
”kumekuwa na malalamiko kutoka kwa chama cha usafirishaji
nchini TABOA kutokana na mzabuni huyo kushindwa kukontroo mwendo mpaka
apige simu makao makuu ilikujua dereva anakwenda mwendo gani”amesema Mhe.Waitara
Aidha ameutaka Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA),kuimarisha shughuli zao na kuboresha utendaji wao ili kukamata soko.
‘Utendaji usio wa kudidhsiha wa TAMESA umefanya kukosa soko la magari ya serikali na ya viongozi na kuwataka kuazia Januria waimarishe utendaji wao”amesema
Aidha, Waitara ameutaka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kuhakikisha wanakamilisha kwa haraka kazi wanazopewa ili kujijengea imani kwa wateja na serikali ambao wanawapa kazi.
Waitara ameitaka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA), kuimarisha hduama wanazozitoa na kuhakikisha wanaimarisha ukaguzi.
“ Hakikisheni minaimarisha ukaguzi, na watu wote lazima wakaguliwe bila kujali aina ya hati za kusafiria, maana suala la usalama wa nchi ni jambo la muimu sana.