Mkurugenzi Mkuu wa TMDA Adam Fimbo (kushoto) akiwa na Meneja Mawasiliano na Elimu kwa Umma Gaudensia Simwanza (kulia) wakiangalia moja ya vipeperushi vinavyotumika katika utoaji wa elimu kwa wananchi wanaotembelea kwenye Banda la Mamlaka hiyo kwenye Maonesho hayo.
Na: Hughes Dugilo, ZANZIBAR.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba Tanzania (TMDA) Adam Fimbo ametoa rai kwa wananchi na jamii kuzingatia matumizi sahihi ya dawa ikiwemo
kuepka matumizi holela ya dawa kwa kutumia dozi kikamilifu sambamba na kupata vipimo na ushauri wa wataalam wa Afya kabla ya kutumia dawa hizo.
Mkurugenzi Fimbo ametoa rai hiyo Disemba 7 mwaka huu alipokuwa katika maonesho ya sekta ya viwanda yanayoendelea kwenye viwanja vya maisala Mjini Zanzibar na kusema kuwa Mamlaka hiyo inandelea kutoa elimu kwa wananchi mbalimbali wanaojitokeza kutembelea kwenye Banda la Mamlaka hiyo kwaajili ya kupata elimu kuhusu shughuli wanazozifanya.
amesema kuwa bado lipo tatizo kwenye jamii ya watanzania kwa baadhi yao kuendelea kutumia dawa pale wanapojisikia kuumwa bila kupima wala kupata ushauri wa Daktari nakwamba imewapelekea kupata madhara zaidi kiafya.
“Bado lipo tatizo katika jamii, watu kutumia dawa kiholela hili ni tatizo ambalo Mamlaka tunaendelea kuwaelimisha wananchi kuwa utumiaji wa dawa kiholela unaweza kusababisha usugu wa bakteria na kufanya dawa hizo kushindwa kufanyakazi ipasavyo” Amesema Fimbo.
Aidha ameongeza kuwa katika Maonesho hayo wanaendelea kutoa elimu juu ya athari za mazumizi ya bidhaa za tumbaku na kuwasisitiza wananchi kuepuka matuzi ya bidhaa hizo ili kuondoa uwezekano wa kupata magonjwa yanatosabiswa na bidhaa hizo.
“Tumbaku ni bidhaa inayoongoza kwa kusababisha magonjwa na vifo kwa watumiaji hivyo hili ni eneo jingine ambalo tumekuwa tukishughulika nalo hapa kwa kutoa elimu kwa wananchi kuwaeleza kwa kina athari zake na kuwashauri kuepuka na kuacha kabisa kuzitumia” ameongeza.
Katika hatua nyingine mkurugenzi huyo alipata fursa ya kutembelea mabanda mbalimbali ya Taasisi nyingine zinazoshiriki maonesho hayo na kuona shughuli wanazofanya sambamba na kushiriki tukio maalum la kula korosho liliondaliwa na kutuo cha utafifiti wa kilimo TARI Naliendele.
Maonesho hayo yanayoendelea Mjini Zanzibar yenye kaulimbiu isemayo “MIAKA 60 TANZANIA IMARA KAZI INDELEE” yanafikia kilele chake Disemba 9 Mwaka huu yakienda sambamba na Shamrashara za kumbukizi ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika ambapo kilele chake ni tarehe 9 Disemba, 2021.
PICHA ZA MKURUGENZI MTENDAJI ADAM FIMBO AKITEMBELEA MABANDA MBALIMBALI.