WAZIRI wa Katiba na Sheria Serekali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Prof. Palamagamba Kabudi, akifungua Kongamano la Maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika, lililofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) kampasi ya Maruhubi.
Washiriki wa Kongamano la Maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika lililofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa Zanzibar (SUZA) kampasi ya Maruhubi
……………………………………………………
Na Judith Mhina -Maelezo
Waziri wa Katiba na Sheria Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Professa Palamagamba Kabudi, amesema kazi kubwa ambayo wanazuoni wanayo ni kufanya utafiti na kuhakikisha wanarithisha historia sahihi lwa watanzania wa vizazi vya sasa na vijavyo.
Profesa labudi ameyasema hayo wakati wa kufumgua kongamano la maadhimisho ya kuelekea kilele cha miaka miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika lililofanyika katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA kampasi ya Maruhubi.
Amesema kazi kubwa inahitajika katika kuhakikisha utafiti wa kina unafanyila kuhusu Historia ya Tanzania, ma sio kujikita kwenye historia ya siasa na uchumi tu na kuacha eneo muhimu la hisrtoria limalohitajika kuwarithisha vijana wa sasa na waabadaye.
“Wazee walio wengi wanajua historia hiyo na kusimulia watoto na wajukuu zao, lakini hawa wazee wakishaondoka kuna hatari ya historia hiyo kupotea kama haikufanyiwa kazi na Wanazuani na kuiweka katika kumbukumbu zitakazo tumika sasa na kwa vizazi vijavyo.” Amesisitiza Kabudi.
Uhuru wa Tanganyika umeleta mshikamano ma ukomavu wa kudu,isha muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao matokeo yake yanaonekana katika kuleta maendleo kwa mwananchi mmoja mmoja, famikia na Taifa kwa ujumla.
Professa Kabudi, amesisiiza kuwa unaposema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ni lazima useme Uhuru wa Tanganyika na Mapinduzi atukufu ya Zanzibar, ambao ndio msingi mkubwa wa Muungano.
“Kongamano hili kimejadili miaka 60 ya uhuru wa Tangayika na tutakaposherekea miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar katika miaka michache ijayo tutakuwa tunajadili chimbuko, shina ambalo matokeo yake ni Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,”,Amesema,
Akelezea historia ya uhuru wa Tanganyika uliofanyika tarehe 9 Desemba mwaka 1961 amesema ni siku muhimu katika historia ya Tanzania kwani Tanganyika ilipata uhuru wake kutoka utawala wa Muingereza ikiwa ni nchi ya udhamini ya Umoja wa Mataifa.
Amesema Watanganyika na Wazanzibar walisherehekea siku hiyo ya Uhuru kwa matumaini ,makubwa ya kujiletea maendeleo, kupata furaha, na ustawi wa jamii husika kijamii, kiuchumi, kisiasa na kimazingira ili kuwa na Taifa bora mambo ambayo walikuwa hawayapati wakati wa kutawaliwa kutokana na mambo mawili makubwa ikiwemo ubeberu,ukoloni na maamuzi ya watu waliohuru kuungana.
Alibainisha kwamba wajerumani walipotawala haukuwa utawala rahimu kwani ndio uliozaa vita vya Majimaji mwaka 1905 mpaka 1907 ukiondoa vita vyengine vya kina Bushiri na wengine pamoja na kushindwa katika vita hivyo lakini vilimfanya mkoloni kuona Watanganyika hawapo tayari kutawaliwa.
Amesema sifa kubwa ya mapambano ya uhuru wa Tanganyika Mwalimu Julias Nyerere alisistiza mambo mbalimbali kwa watanzania ikiwemo kuishi pamoja bila ya kujali, dini, rangi wala kabila.
Akiongelea upande wa Zanzibar pia vitimbi vya ubeberu na ukoloni havikwisha lakini kila njia ilitumika kuhakikisha Zanzibar inabaki katika mikono yao na himaya yao.
Amesema jambo linalowaunganisha watu wa Zanzibar na watu wa Tanganyika katika kupigania uhuru ni kuanzishwa kwa Tanganyika Afrika Association (TAA) Afrika Association Zanzibar na Shirazi Association.
Akiongelea jambo ambalo halifahamiki na wengi ni mchango wa Zanzibar katika kupigania uhuru wa Tanganyika Waziri huyo amesema ni mkubwa kwani watu wengi waliotoka Zanzibar walikwenda kupigania uhuru wao kutokana na udugu walionao.
Kwa upande wa siasa amesema Tanzania imepiga hatua kubwa katika jambo hilo kwani Chama cha Mapinduzi (CCM) ni watu wa mashirikiano, kuafikiana na pia wanaweka maslahi ya wananchi mbele kuliko jambo lolote.
Amesema Tanzania na Zanzibar inapiga hatua kubwa za kimaendeleo hivyo aliwaomba wananchi kubadilika katika kutangaza mafanikio ya nchi yao ikiwemo Zanzibar ambayo ina mafanikio mengi yaliyopatikana.
Sambamba na hayo aliwasihi vijana na wananchi kwa ujumla kuenzi tunu ya amani na utulivu wa nchi yao kwani mambo hayo ndio itakayofanya serikali ya Umoja wa Kitaifa kufanya mambo makubwa zaidi ya kimaendeleo ya leo na vizazi vinavtojuja.
“Kero za Muungano zipo zinatatuliwa na kufanyiwa kazi siku hadi siku na kuzipa ufumbuzi kwa manufaa ya maslahi ya wote”. Amesema Kabudi,
Waziri huyo akizungumzia kauli mbiu ya mwaka huu ya miaka 60 ya uhuru ya ‘Tanzania imara, kazi iendelee’ alisema yapo mambo nane ambayo Tanzania imeyapata katika kipindi hicho cha uhuru ikiwa ni pamoja na tanzania kuwa taifa na sio mkusanyiko wa makabila yasio na umoja katika baadhi ya nchi nyengine zilizokuwepo Afrika.
Jambo jengine alisema inasheherekea miaka 60 ikiwa na Muungano imara usiotetereka wa mataifa mawili huru ambayo kwa hiari yaliamua kuungana, kuadhimisha miaka hiyo ikiwa nchi imeingia uchumi wa kati miaka mitano kabla ya muda uliopangwa katika Tanzania mkuza 2025 na kuwa nchi ya pili ya Afrika Mashatiki na kati wakati wa kipindi kigumu cha ugonjwa wa Uviko 19.
Mafanikio mengine alisema wanasherekea siku hiyo ikiwa Tanzania imara na ikiwa taifa lenye kujiamini kuenzi tunu za Taifa ambazo ni umoja, amani, mshikamano, utu, haki, heshima ya mwanaadamu, uhuru na demokrasia.
Waziri huyo amesema Watanzania wanadhimisha uhuru wa nchi yao wakiwa taifa lenye uthubutu na moyo wa kujitegemea na kujiamini kujenga nchi na kuboresha maisha na ustawi bila ya kumtegemea mtu kwa kushirikiana na mataifa mengine yenye nia njema na maslahi ya nchi.
Sambamba na hayo alisema wanasherekea miaka hiyo wakiwa wameitangazia dunania kuwa utajiri na maliasili zilizokuwepo nchini ni mali ya watanzania, kushihirisha kwamba Kiswahili ambayo ndio lugha iliyotumika kupigania uhuru kuwa lugha ya ukombozi na utambulisho wa hadhi na heshima ya muafrika aliyokuwepo katika bara la Afrika na nje ya Afrika na kuwa lugha ya kimataifa.
Amesema imedhhiirisha dunia ukomavu wa kisiasa na ukomavu wa katiba kwani ni mara ya kwanza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alifariki akiwa madarakani lakini kutokana na katiba iliyoimara madaraka yalihamia kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambayo yalifanyika kwa amani na utulivu.
Aliwaisisitiza watanzania wakati wanasherehekea miaka 60 ya uhuru kuendelea kuwaenzi viongozi wao waliojenga taifa hilo akiwemo Mwalimu Julias Kamabarage Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume.
Amesema mpaka sasa nchi ipo salama katika uongozi imara na madhubuti wa Rais Samia na Dk. Hussein Ali Mwinyi katika kuhakikisha Tanzania inasonga mbele katika kuwaletea wananchi maendeleo.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili, Sera, Uratibu na Baraza la Wawakilishi Dk. Khalid Salum Mohammed, alisema uhuru wa mwaka 1961 Disemba 9 na Mapinduzi ya mwaka 1964 ndio yaliyozaa Muungano wao hivyo wanapaswa kuwakumbuka viongozi wasisi wa uhuru, Mapinduzi na Muungano wa April 26 mwaka 1964 akiwemo Mwalimu Julias Nyerere Hayati Abeid Karume na na wenzao ambao wamefanya kazi kubwa mpaka leo taifa lipo mikono salama.
Alisema uhuru umewapa watanzania heshima ya kujitawala wenyewe na pia umeleta heshima ya kutambulika utu wa watu.
Dk. Khalid alisema Mapinduzi, Muungano na Uhuru umedumishwa katika uongozi wote uliopita hivyo hawana budi kuwapongeza hasa viongozi waliokuwepo hivi sasa madarani ikiwemo Rais Samia kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuendeleza Uhuru, Mapinduzi na Muungano na Rais Mwinyi kwa kuendeleza Mapinduzi na kuiweka nchi katika hali ya amani na utulivu na kuleta maendeleo kwa kasi kubwa zaidi.
Sambamba na hayo aliwataka watanzania kujitambua na kuheshimu historia ya nchi yao.
Mapema Makamu Mkuu wa Chuo cha Taifa Zanzibar (SUZA), Professa Mohammed Makame Haji, alisema kongamano hilo lina lengo kusheherekea miaka 60 ya uhuru na kuakisi Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na Mapinduzi ya mwaka 1964.
Alisema nchi mbili hizo ziliungana sio tu kwa makaratasi bali zilikuwa na udugu wa kidamu hivyo Uhuru na Mapinduzi ndio kielelezo cha udugu uliokuwepo kwa miaka mingi.
Alisema zanzibar ikiwa ni sehemu ya tanzania na ndugu wa tanganyika wameamua kufanya komgamano hilo ili kupata nafasi ya kuona yale mema waliyopata katika uhuru wa Tanganyika na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Katika kongamano hilo mada mbalimbali zilijadiliwa ikiwemo uhuru wa Tanganyik na maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi, miaka 60 ya uhuru wa Tanganyika na Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, mafanikio na changamoto na mwelekeo wa SMZ na SMT katika kuendeleza mafanikio yaliyopatikana na Uhuru wa Tanganyika.
Maadhimisho hayo ambayo yamezundiliwa rasmu Disemba 2 jijini Dodoma ambapo kauli mbiu yake ni ‘Tanzania imara, kazi iendelee’.