Home Mchanganyiko WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI YAWATAKA WATENDAJI MBALIMBALI WA SERIKALI...

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI YAWATAKA WATENDAJI MBALIMBALI WA SERIKALI KUJALI USALAMA WA WAHANGA WA BIASHARA HARAMU YA USAFIRISHAJI BINADAMU

0

Kamishna Msaidizi wa Magereza katika Sekretariet ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu, Ahmad Mwen-dadi akiwasilisha mada ya Usalama na Misaada kwa Wahanga wa Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu kwa watendaji mbalimbali wa Serikali walioshiriki katika mafunzo ya kuwajengea uwezo wa Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu.
Amewataka Watendaji mbalimbali wa serikali walioshiriki katika mafunzo hayo kuzingatia usalama wa wahanga wa biashara haramu ya Usafirishaji Binadamu na kuwaheshimu. Pia amewaomba wasiwahukumu kutokana na hali zao na kuhakikisha wanawapa misaada inayoendana na mahitaji yao.
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupitia Sekretariet ya Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu na TRI (Tanzania Relief Initiative), yanaendelea leo 7/12/2021 ikiwa ni siku ya pili wilayani Kahama, Mkoa wa Shinyanga.

Mwanasheria na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Abdallah Gonzi, akiwasilisha mada ya Namna ya Kuwahoji Wahanga wa Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu kwa watendaji mbalimbali wa Serikali walioshiriki katika Mafunzo  ya kuwajengea uwezo wa Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu leo, 7/12/2021 wilayani Kahama, mkoa wa Shinyanga.
“Usiulize maswali yatakayomuumiza au kumdhalilisha mhanga wa Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu.  Wala kumpa ahadi ambazo huwezi kuzitimiza, mpe uhuru wa kuongea na muda wako ili upate taarifa zaidi zitakazo kusaidia kumsaidia mhanga wa Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu”

Mkurugenzi wa Asasi ya Kiraia, Tanzania Relief Initiatives (TRI) , Edwin Mugambila akiwasilisha mada inayohusu Jitihada zilizochukuliwa na Serikali kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu kwa Watendaji mbalimbali wa Serikali walioshiriki katika Mafunzo ya kuwajengea uwezo wa Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu leo, Desemba 7, 2021, wilayani Kahama, mkoa wa Shinyanga.

Baadhi ya Watendaji na Wadau walioshiriki kwenye Mafunzo ya kuwajengea uwezo wa Kupambana na Kuzuia Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu wakitazama video inayoonesha mfano wa namna Biashara Haramu ya Usafirishaji Binadamu unavyotendeka nchini. Mafunzo hayo yamefanyika leo, Desemba 7, 2021 wilayani Kahama.