Home Biashara KONGAMANO LA DATA TAMASHA 2021,VODACPM TANZANIA PLC KUIFIKIA JAMII KUPITIA HUDUMA ZA...

KONGAMANO LA DATA TAMASHA 2021,VODACPM TANZANIA PLC KUIFIKIA JAMII KUPITIA HUDUMA ZA KIFEDHA,KILIMO NA AFYA

0

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano Vodacom Tanzania PLC, Rosalynn Mworia(katikati )  akichangia mada ya huduma jumuishi za kifedha kwenye kongamano la takwimu (Data Tamasha 2021) kupitia huduma ya M-Pesa, jinsi ambavyo wanafanya malipo kidijitali na kuchangia pato la Taifa. Wengine kulia ni Mike Shaka kutoka Nilipe na Mtaalam wa Taarifa na Takwimu kutoka NMB, Timiebi Itanisa.

Mkuu wa Idara ya  mifumo ya  Kidijitali Vodacom Tanzania PLC (head of digital platform & IOT),  Yvonne Bayona akichangia mada ya Kilimo kupitia Vodacom  M-Kulima kwenye kongamano la takwimu (Data Tamasha 2021) linaloendelea Ndani ya ndaki ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano  (CoICT), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam .

Mkurugenzi wa huduma za Kidijitali Vodacom Tanzania PLC, Nguvu Kamando akichangia mada kwenye kongamano la takwimu (Data Tamasha 2021) jinsi ambavyo Vodacom inaifikia jamii kupata huduma za kidijitali