KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga,akizungumza wakati wa hafla ya kusaini makubaliano ya utendaji baina ya Wizara hiyo na Bodi za Maji za Mabonde iliyofanyika leo Desemba 7,2021 kwenye Ofisi ya Wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba,akizungumza wakati wa hafla ya kusaini makubaliano ya utendaji baina ya Wizara ya Maji na Bodi za Maji za Mabonde iliyofanyika leo Desemba 7,2021 kwenye Ofisi ya Wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga,akisaini mkataba na Kaimu Mkurugenzi Bodi ya Maji Bonde la Wami-Ruvu Mhandisi Elibariki Mmassy wakati wa hafla ya kusaini makubaliano ya utendaji baina ya Wizara hiyo na Bodi za Maji za Mabonde iliyofanyika leo Desemba 7,2021 kwenye Ofisi ya Wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga,akibadilishana mkataba na Kaimu Mkurugenzi Bodi ya Maji Bonde la Wami-Ruvu Mhandisi Elibariki Mmassy mara baada ya kusaini makubaliano ya utendaji baina ya Wizara hiyo na Bodi za Maji za Mabonde iliyofanyika leo Desemba 7,2021 kwenye Ofisi ya Wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga,akisaini Mkataba na Mkurugenzi Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria Renatus Shinhu wakati wa hafla ya kusaini makubaliano ya utendaji baina ya Wizara hiyo na Bodi za Maji za Mabonde iliyofanyika leo Desemba 7,2021 kwenye Ofisi ya Wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga,akibadilishana Mkataba na Mkurugenzi Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria Renatus Shinhu mara baada ya kusaini makubaliano ya utendaji baina ya Wizara hiyo na Bodi za Maji za Mabonde iliyofanyika leo Desemba 7,2021 kwenye Ofisi ya Wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya hafla ya kusaini makubaliano ya utendaji baina ya Wizara hiyo na Bodi za Maji za Mabonde iliyofanyika leo Desemba 7,2021 kwenye Ofisi ya Wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma.
………………………………………………………
Na Alex Sonna, Dodoma
KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga, ameziagiza Bodi tisa za mabonde ya Maji nchini kujipanga kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwenye maeneo yao ili kuwa na rasilimali maji ya kutosha kwa ajili ya wananchi.
Mhandisi Sanga ameyasema hayo leo katika hafla ya kusaini makubaliano ya utendaji baina ya Wizara hiyo na Bodi hizo iliyofanyika kwenye Ofisi ya Wizara hiyo Mtumba jijini Dodoma.
Amesema miongoni mwa maeneo yanayopaswa kuzingatiwa zaidi kwenye utendaji kazi wao ni pamoja na kukabiliana na mabadiliko hayo.
“Mabadiliko haya yanatokea maeneo mengi duniani, sisi ndo walinzi, watunzaji, wasimamizi, wagawaji wa rasilimali hii ya maji, lazima kila mmoja wetu na kila taasisi inayohusika na bonde Fulani iwe na mikakati mahsusi ya kuhakikisha haya yaliyotokea kwa kipindi hichi tuweke nguvu zaidi ya kukabiliana nayo,”amesema.
Amesema kutokana na mabadiliko hayo yaliyokumba baadhi ya maeneo yamesababisha changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji na wananchi kuanza kupata maji kwa njia ya migawo.
“Kwa mfano pale Ruvu maji yalipungua na wananchi wa Dar es salaam na baadhi ya maeneo ya Pwani kupata maji kwa mgawo, hili si jambo la kawaida uwezo upo wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, kikubwa ni kufanya maandalizi ya kutosha yanapotokea yatukute tumejiandaa, kwasababu maji chanzo chake kikubwa ni mvua, zikichelewa kunyesha kunakuwa na ukame,”amesema.
Amesema yanahitajika kujengwa mabwawa ili kutumia fursa ya mvua zinazonyesha kwasasa kwa kuzuia maji kabla hayajaenda baharini hasa kwenye mito inayotiririsha maji kwenda baharini.
Amesisitiza kufanya ukaguzi wa mara kwa mara vibali vya matumizi ya maji kwenye mabonde hayo ili watu watumie kulingana na matakwa ya vibali.
“Pia utunzaji wa vyanzo vya maji, nguvu zaidi ifanyike kwa kuvitambua vyanzo ambavyo havijatambuliwa na kuviwekea mipaka ili vitangazwe kwa mujibu wa sheria ili kulinda maeneo haya yasivamiwe,”amesema.
Kuhusu mikataba iliyosainiwa, Katibu Mkuu huyo amesema husainiwa kila mwaka kwa lengo la kupima utendaji kazi wa bodi hizo.
“Tathmini iliyofanyika ya mwaka 2019/20 inaonesha utendaji ni asilimia 56.2 lakini kwa mwaka 2020/21, ufanisi ni asilimia 75.2, nawapongeza bodi zetu kwa kazi kubwa na nzuri mliyofanya kwa mwaka huu,”amesema.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba
amewataka wahandisi wa mabonde hayo kwenda kutekeleza maagizo waliopewa ili kuweka sekta hiyo imara katika utoaji huduma ya maji.