Amid Shule Kuu ya Uuguzi na Afya kwa Umma, Dk.Stephen Kibusi,akifungua mafunzo ya siku tano ya uimarishaji wa afya kwa wahudumu wa Afya 52 nchini yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto iliyopo ya kuitafsiri sera katika utekelezaji wa suala la afya jamii yaliyoanza leo Desemba 6,2021 jijini Dodoma.
Meneja Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS) ,Ally Kebby ,akieleza jinsi walivyoamua kutoa mafunzo kwa wahudumu wa Afya 52 nchini yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto iliyopo ya kuitafsiri sera katika utekelezaji wa suala la afya jamii yaliyoanza leo Desemba 6,2021 jijini Dodoma.
Mratibu wa Huduma za Afya ya Jamii kutoka Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Martha Mariki,akizungumza wakati wa mafunzo ya siku tano ya uimarishaji wa afya kwa wahudumu wa Afya 52 nchini yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto iliyopo ya kuitafsiri sera katika utekelezaji wa suala la afya jamii yaliyoanza leo Desemba 6,2021 jijini Dodoma.
Mkuu wa Idara ya Afya kwa Umma Dk.Leonard Katalambula,akizungumza wakati wa mafunzo ya siku tano ya uimarishaji wa afya kwa wahudumu wa Afya 52 nchini yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto iliyopo ya kuitafsiri sera katika utekelezaji wa suala la afya jamii yaliyoanza leo Desemba 6,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia ufunguzi wa mafunzo ya siku tano ya uimarishaji wa afya kwa wahudumu wa Afya 52 nchini yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto iliyopo ya kuitafsiri sera katika utekelezaji wa suala la afya jamii yaliyoanza leo Desemba 6,2021 jijini Dodoma.
Meneja Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS) ,Ally Kebby,akimkabidhi Amid Shule Kuu ya Uuguzi na Afya kwa Umma, Dk.Stephen Kibusi vifaa mbalimbali vya kufundishia na kujifunzia UDOM vyenye thamani ya Sh. Milioni 21 ili kuboresha kazi ya kutoa mafunzo ya afya na utafiti wakati wa mafunzo kwa wahudumu wa Afya 52 nchini leo Desemba 6,2021 jijini Dodoma.
Meneja Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS) ,Ally Kebby,akionyesha vifaa mbalimbali vya kufundishia na kujifunzia UDOM vyenye thamani ya Sh. Milioni 21 ili kuboresha kazi ya kutoa mafunzo ya afya na utafiti mara baada ya kukabidhi vifaa hivyo wakati wa mafunzo kwa wahudumu wa Afya 52 nchini leo Desemba 6,2021 jijini Dodoma.
Amid Shule Kuu ya Uuguzi na Afya kwa Umma, Dk.Stephen Kibusi,akimshukuru Meneja Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS) ,Ally Kebby mara baada ya kupokea vifaa mbalimbali vya kufundishia na kujifunzia UDOM vyenye thamani ya Sh. Milioni 21 ili kuboresha kazi ya kutoa mafunzo ya afya na utafiti wakati wa mafunzo kwa wahudumu wa Afya 52 nchini leo Desemba 6,2021 jijini Dodoma.
Meneja Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS) ,Ally Kebby,akimsikiliza Mkuu wa Idara ya Afya kwa Umma Dk.Leonard Katalambula mara baada ya kukabidhiwa vifaa mbalimbali vya kufundishia na kujifunzia UDOM vyenye thamani ya Sh. Milioni 21 ili kuboresha kazi ya kutoa mafunzo ya afya na utafiti.Kushoto ni Amid Shule Kuu ya Uuguzi na Afya kwa Umma, Dk.Stephen Kibusi
Amid Shule Kuu ya Uuguzi na Afya kwa Umma, Dk.Stephen Kibusi,(katikati) pamoja na Meneja Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS) ,Ally Kebby (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya siku tano ya uimarishaji wa afya kwa wahudumu wa Afya 52 nchini yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto iliyopo ya kuitafsiri sera katika utekelezaji wa suala la afya jamii yaliyoanza leo Desemba 6,2021 jijini Dodoma.
………………………………………………….
Na Alex Sonna, Dodoma
WAHUDUMU wa Afya 52 kutoka mikoa 26 nchini wamepewa mafunzo ya siku tano ya uimarishaji wa afya yenye lengo la kuwajengea uwezo wa kukabiliana na changamoto iliyopo ya kuitafsiri sera katika utekelezaji wa suala la afya jamii.
Mafunzo hayo yanatolewa na Mradi wa HPSS – Tuimarishe Afya unaofadhiliwa na Serikali ya Uswisi kupitia Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi (SDC) na unaotekelezwa na Taasisi ya Uswisi ya Tropical and Public Health (Swiss TPH), kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
Akizungumza leo Desemba 6,2021 jijini Dodoma katika mafunzo hayo,Meneja Mradi wa HPSS-Tuimarishe Afya, Ally Kebby amesema mafunzo hayo yamewashirikisha waratibu wa afya wa mikoa 26 na waratibu 26 wa uimarishaji afya wa shule za mikoa nchi nzima ambayo yanalenga kufundisha mbinu shirikishi za kuimarisha afya katika jamii na shuleni kwa kuwajengea uwezo watumishi wa afya kutoka vituo vya afya vya umma kote nchini.
“Katika kuchangia juhudi za serikali katika kutoa huduma bora za afya kwa wananchi wake, mradi wa HPSS-Tuimarishe afya kwa kushirikiana na UDOM tunatoa mafunzo haya ambayo yanahusu mbinu mbalimbali shirikishi zinazolenga kuziwezesha jamii kuchukua udhibiti wa afya na ustawi wao,”amesema.
Meneja huyo amesema pamoja ufadhili wa mafunzo hayo pia kupitia mradi huo wametoa vifaa mbalimbali vya kufundishia na kujifunzia UDOM vyenye thamani ya Sh. Milioni 21 ili kuboresha kazi ya kutoa mafunzo ya afya na utafiti.
Bw.Kebby amevutaja vifaa hivyo ni pamoja na Kompyuta Mpakato 3,Projekta,Skrin ya Projekta,Printa na mashine ya kunakili,vitabu vya kumbukumbu,vitavu,ubao mweupe na ubao wa kubadindika matangazo
Amebainisha kuwa mafunzo hayo yatasaidia wahudumu hao kuongeza ujuzi katika kupanga bajeti kutekeleza na kusimamia afua za uhamasishaji wa afya ya jamii na shuleni.
Akifungua mafunzo hayo Amid Shule Kuu ya Uuguzi na Afya kwa Umma, Dk.Stephen Kibusi amesema mafunzo hayo yatasaidia kuwawezesha waratibu kubeba ajenda za afya ya jamii.
Amesema serikali imejizatiti kuhakikisha kuwa watu wanakuwa salama dhidi ya magonjwa yanayozuilika na kuepukika ili kuchangia maendeleo ya uchumi wa taifa.
Awali,Mratibu wa Huduma za Afya ya Jamii kutoka Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),Martha Mariki amesema mafunzo hayo ni muhimu sana kwao.
Ushirikiano kati ya mradi wa HPSS –Tuimarishe Afya na UDOM ulianza mwaka 2014 na unalenga kusaidia serikali katika kukabiliana na upungufu wa watumishi wa afya hasa katika eneo la kuimarisha afya.