Home Siasa KUMBUKIZI MIAKA 20 KIFO CHA BRIG. JENERALI MOSES NNAUYE YAKUTANISHA MAGWIJI WA...

KUMBUKIZI MIAKA 20 KIFO CHA BRIG. JENERALI MOSES NNAUYE YAKUTANISHA MAGWIJI WA SIAZA ZA TANZANIA

0

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza viongozi mbali mbali wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar, waasisi wa TANU na ASP, wakuu wa vyombo vya ulinzi na Usalama wastatafu, Waziri Mkuu Mstaafu Joseph Sinde Warioba, Mawaziri Wastaafu, Makatibu Wakuu Wakuu Wastaafu wa CCM (Kanali Abdulrahman Kinana, Mzee Yusuf Makamba na Wilson Mkama), Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka, Wabunge na viongozi kadhaa wa vyama vya siasa Jumapilli 5 Desemba, 2021, Wamehudhuria Kongamano Maalum la kumbukizi ya Miaka 20 ya kifo cha Marehemu Brig. Jenerali. Moses Nnauye yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere Dar es Salaam.

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Daktari Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza katika kongamano hilo kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Balozi Ombeni Sefue, na kushoto ni Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Kanali Abdulrahman Kinana.

Nape Nnauye Mbunge wa jimbo la Mtama mkoani Lindi ambaye ni Mtoto wa Hayati Brig. Jenerali Moses Nnauye kulia akiwa na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Shaka Hamdu Shaka wakijadiliana jambo katika kongamano hilo.

Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Kanali Abdulrahman Kinana akizungumza katika kongamano hilo.

Nape Nnauye Mbunge wa jimbo la Mtama mkoani Lindi ambaye ni Mtoto wa Hayati Brig. Jenerali Moses Nnauye kulia akiteta jambo na Naibu Waziri wa Kilimo Mh. Hussein Bashe.

Katibu Mkuu mstaafu wa CCM Mzee Yusuf Makamba akiwa na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee Joseph Sinde Warioba katika kongamano hilo.

Katibu Mkuu mstaafu wa CCM Mzee Yusuf Makamba akitoa mchango wake katika kongamano hilo.

Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Kanali Abdulrahman Kinana akizungumza na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM Taifa Ndugu Shaka Hamdu Shaka katika kongamano hilo.

Viongozi mbalimbali wakiwa katika kongamano hilo.