WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso,akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mwanahamisi Munkunda kabla ya kuzindua programu ya kusukuma maji kwa kutumia nishati ya umeme jua katika Kijiji cha Zanka, Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.
WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu ya kusukuma maji kwa kutumia nishati ya umeme jua katika Kijiji cha Zanka, Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma ambapo mradi huo utanufaisha jumuiya za maji vijijini 125 ambazo zinahudumia vijiji 215 vyenye zaidi ya wakazi 560,000 katika Wilaya 25.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mwanahamisi Munkunda,akizungumza wakati wa uzinduzi wa Programu ya kusukuma maji kwa kutumia nishati ya umeme jua katika Kijiji cha Zanka, Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma ambapo mradi huo utanufaisha jumuiya za maji vijijini 125 ambazo zinahudumia vijiji 215 vyenye zaidi ya wakazi 560,000 katika Wilaya 25.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Tanzania (TIB), Charles Singili,akizungumza kwenye uzinduzi wa Programu ya kusukuma maji kwa kutumia nishati ya umeme jua katika Kijiji cha Zanka, Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma ambapo mradi huo utanufaisha jumuiya za maji vijijini 125 ambazo zinahudumia vijiji 215 vyenye zaidi ya wakazi 560,000 katika Wilaya 25.
Kaimu Mkurugenzi wa RUWASA, Mhandisi Mkama Bwire,akizungumza kwenye uzinduzi wa Programu ya kusukuma maji kwa kutumia nishati ya umeme jua katika Kijiji cha Zanka, Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma ambapo mradi huo utanufaisha jumuiya za maji vijijini 125 ambazo zinahudumia vijiji 215 vyenye zaidi ya wakazi 560,000 katika Wilaya 25.
Mbunge wa Jimbo la Bahi Kenneth Nollo,akizungumza kwenye uzinduzi wa Programu ya kusukuma maji kwa kutumia nishati ya umeme jua katika Kijiji cha Zanka, Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma ambapo mradi huo utanufaisha jumuiya za maji vijijini 125 ambazo zinahudumia vijiji 215 vyenye zaidi ya wakazi 560,000 katika Wilaya 25.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Programu ya kusukuma maji kwa kutumia nishati ya umeme jua katika Kijiji cha Zanka, Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma ambapo mradi huo utanufaisha jumuiya za maji vijijini 125 ambazo zinahudumia vijiji 215 vyenye zaidi ya wakazi 560,000 katika Wilaya 25.
Waziri wa Maji Jumaa Aweso,akimsikiliza Meneja wa RUWASA Wilaya ya Bahi Robert Mgombela wakati akimuonyesha mchoro wa Programu ya kusukuma maji kwa kutumia nishati ya umeme jua katika Kijiji cha Zanka, Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma ambapo mradi huo utanufaisha jumuiya za maji vijijini 125 ambazo zinahudumia vijiji 215 vyenye zaidi ya wakazi 560,000 katika Wilaya 25.
WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso,akizindua Programu ya kusukuma maji kwa kutumia nishati ya umeme jua katika moja ya kituo cha kuchotea maji kilichofungwa dira inayotumia mfumo wa malipo kabla katika Kijiji cha Zanka, Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma ambapo mradi huo utanufaisha jumuiya za maji vijijini 125 ambazo zinahudumia vijiji 215 vyenye zaidi ya wakazi 560,000 katika Wilaya 25.
Waziri wa Maji,Jumaa Aweso akimtwisha ndoo ya maji Anna Male Mkazi wa kijiji cha Zanka baada ya kuchota maji kwa kutumia tokeni kwenye moja ya kituo cha kuchotea maji kilichofungwa dira inayotumia mfumo wa malipo kabla.
Waziri wa Maji,Jumaa Aweso ,akiwanyoshea mkono wanakijiji (hawapo pichani) baada ya kumtwisha ndoo ya maji Anna Male Mkazi wa kijiji cha Zanka baada ya kuchota maji kwa kutumia tokeni kwenye moja ya kituo cha kuchotea maji kilichofungwa dira inayotumia mfumo wa malipo kabla.
Waziri wa Maji,Jumaa Aweso,akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mwanahamisi Munkunda baada ya kuzindua programu ya kusukuma maji kwa kutumia nishati ya umeme jua katika moja ya kituo cha kuchotea maji kilichofungwa dira inayotumia mfumo wa malipo kabla katika Kijiji cha Zanka, Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.
Waziri wa Maji,Jumaa Aweso akimsikiliza mwenyekiti wa chombo cha watoa huduma ya maji ngazi ya jamii Zanka-Zanka CBWSO,Pelis Mele (wa tatu kushoto) juu ya namna ya kutumia tokeni kwenye moja ya kituo cha kuchotea maji kilichofungwa dira inayotumia mfumo wa malipo kabla katika kijiji cha Zanka.
Waziri wa Maji,Jumaa Aweso,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua programu ya kusukuma maji kwa kutumia nishati ya umeme jua katika Kijiji cha Zanka, Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma ambapo mradi huo utanufaisha jumuiya za maji vijijini 125 ambazo zinahudumia vijiji 215 vyenye zaidi ya wakazi 560,000 katika Wilaya 25.
……………………………………………………………..
Na Alex Sonna, Bahi
WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amezindua programu ya kusukuma maji kwa kutumia nishati ya umeme jua katika Kijiji cha Zanka, Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma na kubainisha kuwa teknolojia hiyo itapunguza gharama za uendeshaji miradi ya maji.
Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Aweso amesema hatua hiyo ni matokeo ya utafiti uliofanyika mwaka 2015 uliohusu namna ya kutumia nishati ya jua katika kusukuma maji.
“Mradi huu unatekelewa katika mikoa mitano ya Singida, Dodoma, Mtwara, Shinyanga na Tabora na umegharimu Dola za Marekani milioni 7.3,”amesema.
Amebainisha kuwa mradi huo utanufaisha jumuiya za maji vijijini 125 ambazo zinahudumia vijiji 215 vyenye zaidi ya wakazi 560,000 katika Wilaya 25.
Hata hivyo, alizitaka Mamlaka za maji nchini kuweka uwiano sawa wa unit za maji katika maeneo ya mijini na vijijini ili kuondoa ukakasi uliopo ambapo wanalipishwa fedha nyingi.
“Inashangaza katika miradi yetu ya maji vijijini, niliwahi kuwahoji inakuwaje mtu wa Dar es Salaam akalipa uniti za maji kwa sh. 1250 halafu huku mtu wa vjijini analipa zaidi ya sh. 5000,”amesema.
Amesisitiza matumizi ya teknolojia ya kufanya mabadiliko na kupunguza mzigo mzito ambao wananchi wa vijijini wanabebeshwa.
“Nilipata taarifa eneo la Bahi linasimamiwa na Ruwasa uniti moja hapa mnauza sh. 2500, Ruwasa mjini mnauza uniti kwa sh.1340, hapana mimi mambo hayo ndio siyataki mnatuletea ukakasi kwani DUWASA ya Bahi na ya Dodoma mnatofautiana nini,”amehoji.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mwanahamisi Munkunda,amesema kuwa wataweka usimamizi madhubuti wa miradi yote ya maji hasa mradi wa malipo kabla kwa kuwa viongozi wote katika wilaya yake wameuelewa.
”Manufaa ya mradi huo ni kusongeza huduma ya maji kwa wananchi na kuimarisha usimamizi wa mapato na matumizi ya fedha zinazopatikana kutokana na makusanyo ya mauzo ya maji”amesema
Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo Tanzania (TIB), Charles Singili amesema mradi huo wa kusukuma maji kwa kutumia nishati ya umeme jua ulibuniwa kutokana na utafiti uliofanywa mwaka 2015 kwa ufadhili wa Benki ya Dunia (WB) kuangalia namna ya kusaidia jumuiya za maji vijijini ambazo zilionekana kukosa uendelevu.
Amesema hatua hiyo ilisababishwa na mzigo mkubwa wa gharama za uendeshaji hasa ununuzi wa dizeli, kuharibika mara kwa mara kwa mitambo ya kusukuma maji pamoja na ufanisi mdogo katika ukusanyaji mapato ya mauzo ya maji.
Naye, Kaimu Mkurugenzi wa RUWASA, Mhandisi Mkama Bwire amesema miradi ya maji inayotumia teknolojia hiyo itasaidia kuondoa changamoto ya gharama kubwa ya maji tofauti na miradi inayotumia dizeli.