- Wateja kushinda zawadi kwa kutumia huduma za Vodacom na kugawana na familia na marafiki
- Kampeni inalenga kuwezesha sherehe za wateja katika kipindi hiki cha sikukuu
- Kampeni inahusisha mtu maalum – ‘Masta Shangwe’ atakayekuwa akigawa zawadi za papo hapo
3 Disemba 2021 – Dar es Salaam. Vodacom Tanzania Plc, kampuni ya teknolojia na mawasiliano inayoongoza nchini leo imezindua kampeni yake ya msimu wa siku kuu inayoitwa “Show Love, Tule Shangwe” inayolenga kuwezesha watumiaji wake kushinda zawadi kadha wa kadha ikiwa ni pamoja na; televisheni, simu janja na pesa taslimu. Ili kunogesha na ushirikiano katika kipindi hiki cha sikukuu, wateja watagawana zawadi hizi na wapendwa wao.
Akiongea wakati wa uzinduzi, Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Sitholizwe Mdlalose alisema, “Nina furaha kubwa kuwatangazia uzinduzi wa kampeni hii ya Vodacom – ‘Show Love, Tule Shangwe’. Kampeni hii inaendana na dhamira ya upendo na ushirkiano. Tuliwaahidi kuwa ‘Yajayo yanafurahisha’ na leo, kupitia uzinduzi huu tunathibitisha msemo wa vodaom kuwa ‘Pamoja Tunaweza’ ambao unasisitiza jinsi ambavyo ushirikiano kati ya utu na ubinadamu na ubunifu unavyoweza kuzaa matunda makubwa.”
Kampeni hii ya wiki 6 itakuwa na uwepo wa mtu maalum aitwaye “Masta Shangwe” – atakayejitokeza hapa na pale nchi nzima kuwazawadia wateja wa Vodacom zawadi nyingi za papo hapo.
“Masta Shangwe atakuwepo kuwazawadia wateja wetu walioishi Maisha ya kidijitali, kutakuwa na zawadi za papo hapo kwa wateja pindi watumiapo huduma kama vile M-Pesa na App ya ‘My Vodacom” kusambaza upendo kwa familia na marafiki kwa njia ya kutuma pesa au kuwanunulia bando za mawasiliano” alisema Sitholizwe.
Akielezea zaidi jinsi watumiaji watakavyonufaika na kampeni hii, Linda Riwa, Mkurugenzi wa Biashara wa Vodacom Tanzania alisema, “Wakati huu, watu wengi husherehekea kwa kukusanyika kifamilia, kununua na kupeana zawadi na kusafiri mikoani. Kwetu Vodacom, tunataka kuwezesha wateja wetu kusherehekea msimu huu kupitia bidhaa na huduma zetu. Wateja watahitajika kutumia huduma zetu. Kama vile kumnunulia bando Rafiki au kugawa sehemu ya bando baada ya kujinunulia mwenyewe; Kufanya miamala kupitia M-Pesa kama kulipia huduma au kumtumia mtu pesa; Kucheza mchezo wa “Tikisa Ushinde” au kujisajili huduma ya POA TV.“
Kampeni hii imepangwa kuendelea hadi mwezi wa kwanza mwakani na kutakuwa na zawadi za kila siku, wiki, mwezi na pia kutakuwa na zawadi kuu. Zawadi hizo ni pamoja na:
- Kurejeshewa Pesa kwenye akaunti ya M-Pesa baada ya kulipia huduma
- Muda wa maongezi
- Bidhaa za nyumbani
- Simu za mkononi
- Malipo ya LUKU
- Vifurushi vya DSTV
- Kulipiwa tiketi ya usafiri mikoani
- Vocha za kununulia bidhaa madukani
- Malipo ya ada za shule.
Ili kushiriki na kusambaza upendo, wateja watapiga *149*01# au watatumia App ya M-Pesa, wataingiza tamanio na namba za simu za ndugu au marafiki wanaotaka kugawana nao zawadi.
Kuhusu Vodacom Tanzania PLC
Vodacom Tanzania PLC ni kampuni inayoongoza ya huduma za mawasiliano ikiwa na mtandao wenye kasi kubwa zaidi wa data nchini. Tunatoa huduma za mawasiliano kwa watumiaji zaidi ya milioni 15. Vodacom Tanzania na kampuni zake ni sehemu ya Vodacom Group iliyosajiliwa nchini Afrika Kusini ambayo yenyewe inamilikiwa na Vodafone Group ya nchini Uingereza. Imesajiliwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE) ikiwa na namba ya usajili ISIN:TZ1886102715 Jina la Hisa: VODA