Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akiangalia ramani ya ujenzi wa jengo jipya la ghorofa sita la Wizara yake, awamu ya pili katika Mji wa Serikali, Mtumba, jijini Dodoma, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya awali ya ujenzi huo, leo Desemba 3, 2021. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima. Jengo hilo linatarajiwa kukamilika Oktoba 14, 2023
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akimpa maelekezo Mshauri Elekezi, Peter Salyeem (kushoto) wa ujenzi wa jengo jipya la ghorofa sita la Wizara yake, awamu ya pili katika Mji wa Serikali, Mtumba, jijini Dodoma, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya awali ya ujenzi huo, leo Desemba 3, 2021. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima. Jengo hilo linatarajiwa kukamilika Oktoba 14, 2023.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza jambo na Mkurugenzi wa Ujenzi na Uhandisi wa Shirika la Nyumba Tanzania (NHC), Haikamen Mlekio (kushoto) ambaye ni Mkandarasi wa ujenzi wa jengo jipya la ghorofa sita la Wizara yake, awamu ya pili katika Mji wa Serikali, Mtumba, jijini Dodoma, alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya awali ya ujenzi huo, leo Desemba 3, 2021. Watatu kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima. Jengo hilo linatarajiwa kukamilika Oktoba 14, 2023.
Muonekano wa jengo jipya la ghorofa sita la Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi litakapokamilika katika Mji wa Serikali, Mtumba, jijini Dodoma, Oktoba 14, 2023.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene akizungumza jambo na Naibu Katibu Mkuu, Ramadhani Kailima (kushoto), baada ya kumaliza kukagua maendeleo ya awali ya ujenzi wa jengo jipya la ghorofa sita la Wizara yake, awamu ya pili katika Mji wa Serikali, Mtumba, jijini Dodoma, leo Desemba 3, 2021. Katikati ni Msajili wa Jumuiya wa Wizara hiyo, Emmanuel Kihampa. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.