Kamishna wa Maadili Jaji wa Rufani Mhe.Sivangilwa Mwangesi,wakati akitoa taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Desemba 3,2021 katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili jijini Dodoma.
Kamishna wa Maadili Jaji wa Rufani Mhe.Sivangilwa Mwangesi,akisisitiza jambo kwa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Desemba 3,2021 wakati akitoa taarifa katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili jijini Dodoma.
Waandishi wa habari wakimsikiliza Kamishna wa Maadili Jaji wa Rufani Mhe.Sivangilwa Mwangesi,wakati akitoa taarifa leo Desemba 3,2021 katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili jijini Dodoma.
…………………………………………………………..
Na.Erick Mungele,Dodoma
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amerejesha Tamko lake la Raslimali na Madenikatika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya viongozi wa Umma.
Hayo yamesemwa leo Desemba 3,2021 jijini Dodoma na Kamishna wa Maadili Jaji wa Rufani Mhe.Sivangilwa Mwangesi wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili,ambapo amesema kuwa Rais Samia kwa kuonyesha anaongoza kwa vitendo.
“Tunajua Mhe. Rais ana majukumu mengi lakini ameweza kulitekeleza takwa hilo la kikatiba na kisheria kikamilifu”.
Aidha Mheshimiwa Mwangesi ametoa wito kwa Viongozi wote wa Umma wanaowajibika na Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma kurejesha matamko yao kwawakati ambapo amesema kuwa Kiongozi anatakiwa kurejesha tamko lake kabla au ifikapo tar 31 Desemba.
“Kama Rais wa nchi ametekeleza takwa hilo la kikatiba na kisheria kwa wakati nawasihi viongozi wengine kufanya hivyo kwani umebaki mwezi mmoja tu mpaka kufikia tarehe ya mwishoya kutekeleza takwa hilo kwa mujibu wa sharia”.
Kwa mujibu wa Mhe. Mwangesi Kiongozi wa umma kutorejesha Tamko la Rasilimali na Madeni ni kosa kwa mujibu wa kifungu cha 15 cha Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995.
Mhe. Mwangesi amezitaja hatua zinazoweza kuchukuliwa kwa kiongozi wa umma ambaye atashindwa kutekeleza takwa hilo la kisheria ni pamoja na kutakiwa kutoa sababu na inapobainika kuwa sababu alizozitoa sio za msingi basi Sekretarieti ya Maadili humfikisha kiongozi huyo mbele ya Baraza la Maadili.
Amefafanua kuwa hadi kufikia tarehe 30 mwezi Novemba jumla ya Viongozi 161kati ya Viongozi zaidi ya 15,000 wanaopaswa kutoa matamko walikuwa wamerejesha matamko yao na kwamba idadi hiyo ni ndogo ikilinganishwa na idadi ya viongozi wote wanaotakiwa kurejesha matamko yao.
Aidha maesema kuwa ni takwa la Kisheria kwa Kiongozi wa Umma kurejesha Tamko la Raslimali na Madeni yake kuanzia tarehe1 Octoba hadi tarehe 30 Desemba kila mwaka.
Hata hivyo Mhe. Mwangesi ametumia hiyo kuujulisha umma juu ya tukio la Maadhimisho ya Siku ya Maadili Duniani ambayo kitaifa yatafanyika Jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 10 Desemba, 2021.