Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka akigawa mipira na jezi kwa timu nne za soka zilizopo katika kata ya mail moja.
…………………………………………………………..
Na Victor Masangu,Kibaha
Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka katika kutekeleza Ilani ya Chama Cha mapinduzi CCM ya kukuza sekta ya michezo kwa vijana ametoa jezi na mipira kwa timu nne za soka zilizopo kata ya mail moja.
Koka ametoa vifaa hivyo vya michezo ikiwa ni moja ahadi yake ambayo aliitoa wakati wa ziara yake ya kampeni kwa ajili ya kuwaomba kura wananchi wa kata ya mail moja ili aweze kuwaletea mabadiliko chanya ya kimaendeleo ikiwemo kukuza michezo.
Koka ametekeleza ahadi hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi yenye lengo la kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo pamoja na kusikiliza kero na changamoto ambazo zinawakabili ili aweze kuzichukua na kuzitafutia ufumbuzi.
Mbunge Koka alisema kwamba nia yake kubwa ni kuhakikisha anaweka mipango madhubuti ya kukuza sekta ya michezo kuanzia ngazi za chini kwa vijana ili waweze kutimiza malengo ambayo wamejiwekea.
Pia alibaisha kuwa katika Jimbo lake ya Kibaha mji anatambua kuwa Kuna wachezaji wengi ambao wanavipaji kutoka kata zote 14 hivyo lengo lake ni kuwaendeleza zaidi katika kutimiza ndoto zao.
Katika ziara hiyo Mbunge huyo ambaye aliambatana na viongozi mbali mbali wa serikali,wakuu wa idara pamoja na baadhi ya viongozi wa timu zote nne za soka zilizopo kata ya mail moja.
Timu nne za soka ambazo zimeweza kufanikiwa kupata jezi na mipira kutoka kwa MBunge Koka ni pamoja na Sober FC,Mail moja,na Black mamba.