Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro Disemba 3, 2021 ameongoza kikao cha Utendaji kazi cha Maofisa Wakuu wa Makao Makuu ya Polisi jijini Dodoma, kujadili utendaji wa kazi za Jeshi hilo, kufanya tathmini ya mafanikio yaliyopatikana, changamoto kwa kipindi kilichopita na kuweka mikakati ya kutekeleza kazi za Polisi kwa ufanisi katika kulinda usalama wa raia na mali zao.