Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge (kulia)
akikata utepe kuzindua hafla fupi ya utiaji saini wa mikataba ya ujenzi na
matengenezo ya Barabara kati ya Wakandarasi na Wakala wa Barabara za Vijijini
na Mijini (TARURA) mkoani singida leo Tarehe 1 Desemba 2021. Wengine katikati
ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida Juma Kilimba na Mratibu wa Tarura Mkoa wa
Singida, Mhandisi Tembo Davascar.
Dkt Mahenge akionyesha mwonekano wa mkataba huo.
Mahenge akizungumza kwenye hafla hiyo.
wa CCM Mkoa wa Singida Juma Kilimba akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mratibu wa Tarura Mkoa wa Singida, Mhandisi Tembo Davascar
akitoa taarifa fupi ya mwenendo mzima wa zoezi hilo.
mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla hiyo.
mbalimbali wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa hafla hiyo.
la Utiaji saini wa mikataba hiyo likiendelea.
Godwin Myovela, Singida
ZAIDI ya shilingi 12 bilioni zimetolewa na serikali kwa
idadi ya kandarasi 26 kwa ajili ya matengenezo ya barabara za vijijini mkoani
hapa.
Mpaka sasa mikataba 26 ya matengenezo ya barabara hizo yenye
thamani ya shilingi bilioni 12.6 tayari imesainiwa kati ya Wakandarasi na
Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini mkoani hapa (TARURA) huku Mkuu wa Mkoa
Dkt. Binilith Mahenge na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM, mkoa wa
Singida Alhaji Juma Kilimba wakishuhudia
zoezi hilo.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mratibu wa Tarura mkoa wa
Singida, Mhandisi Tembo Davascar, alisema mikataba hiyo 26 ya awamu ya pili
itahusisha matengenezo na ujenzi wa barabara zilizopo wilaya za Ikungi,
Manyoni, Mkalama, Itigi, Iramba na Singida Vijijni.
Hata hivyo, Davascar alisema wametoa siku 14 kuanzia sasa
kwa wazabuni hao kujipanga na kuandaa vikosi kazi vyao na baada ya hapo
watatakiwa kutekeleza mikataba yao ndani ya kipindi kisichozidi miezi 6 baada
ya siku hizo
“Ratiba ya utekelezaji wa hii mikataba itaanza siku 14
kuanzia sasa, na kuanzia Desemba 15 wanapaswa kuanza mara moja utekelezaji wa
mkataba kwa kipindi kisichopungua miezi 6,” alisema.
Awali akizungumza kabla ya zoezi la utiaji saini, Dkt
Mahenge aliwahimiza na kuwakumbusha wakandarasi kuzingatia kikamilifu ratiba ya
utekelezaji wa mikataba hiyo bila ya kuingiza visingizio vyovyote vinavyoweza
kukwamisha ustawi wa miradi hiyo muhimu kwa maendeleo
Aidha, alisisitiza juu ya umuhimu wa kuzingatia ubora na
viwango sambamba na kutanguliza uzalendo wakati wa utekelezaji wake kulingana
na thamani ya fedha zilizotolewa ambazo ni chimbuko la kodi za wananchi katika
muktadha chanya wa matumizi endelevu kwa vizazi vya sasa na baadaye.
“Nikiwatazama wahandisi wote hapa mnaosaini mikataba ya
ujenzi wa barabara hizi ni wazawa, sitarajii kuona virusi vyovyote vinajitokeza
wakati wa utekelezaji wa miradi hii ambayo Mheshimiwa Rais ameamua bilioni hizi
12.6 zielekezwe kwetu kwa ajili ya barabara za vijijini pekee…naomba
tusimwangushe, na tusiwaangushe walipa kodi waliowezesha hili kufanyika,”
alisema Dkt. Mahenge
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)
Mkoa wa Singida, Alhaji Juma Kilimba, akiwa miongoni mwa walioshuhudia zoezi la
utiaji saini alipongeza serikali kupitia chama hicho kwa kutekeleza yale
yalioelekezwa kwenye ilani
“Hakikisheni fedha zilizotolewa zinakwenda kutumika kwa
malengo yaliyokusudiwa…nawasihi sana wakandarasi msiende kuboronga, mana kama
mtaharibu ahadi hizi ambazo chama na serikali tuliahidi kwa wananchi mjue
mwisho wa siku atakayelaumiwa na kupigwa mawe ni sisi chama na sio ninyi,”
alisema Kilimba.