Timu ya Chelsea imeendelea na wimbi la ushindi baada ya kupata kuwachapa wenyeji Watford mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Vicarage Road mjini Watford.
Mabao ya Chelsea yalifungwa na Mason Mount dakika ya 29 na Hakim Ziyech dakika ya 72, wakati la Watford lilifungwa na Emmanuel Dennis 43.
Kwa ushindi huo Chelsea inaendelea kuongoza Ligi wakiwa na pointi 33 pointi moja zaidi ya Manchester City na mbili zaidi ya Liverpool baada ya timu zote kucheza mechi 14, wakati Watford inabaki na pointi zake 13 za mechi 14 nafasi ya 17.