Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) Salum Yussuf Ali, akizungumza katika kikao cha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Jamali Kassim Ali, (hayupo pichani) kinachohusu mfumo wa VFMS, hafla iliyofanyika Ukumbi wa ZRB Mazizini Mjini Zanzibar.
Kaimu Mkurugenzi ICT (Tehama) kutoka Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) Harith Abdil – azizi Ahmada akitoa ripoti ya ulipaji kodi katika kikao cha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Jamali Kassim Ali, kinachohusu mfumo wa VFMS, hafla iliyofanyika Ukumbi wa ZRB Mazizini Mjini Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Jamali Kassim Ali,wa kwanza (kushoto) pamoja na Wafanyakazi wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) wakiangalia ripoti ya ulipaji kodi iliyowasilishwa kwa njia ya mtandao, katika kikao cha Waziri wa Fedha na Mipango Jamali Kassim Ali, kinachohusu mfumo wa VFMS, hafla iliyofanyika Ukumbi wa ZRB Mazizini Mjini Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Jamali Kassim Ali wa ( katikati) akiangalia Mtazamo mzima wa uingiaji wageni na ulipaji kodi katika Hoteli ya Madinatul-Bahar, huko Mbweni Mjini Zanzibar.
Mfanyabiashara wa Duka la Saleh Decoration liliopo Miembeni Mkoa wa Mjini ,Hassan Saleh Ashuor , akimtolea risiti Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Jamali Kassim Ali kwa kutumia mashine ya VFMS.
Picha Na Maryam Kidiko / Maelezo Zanzibar.
……………………………………………………………..
Na kijakazi Abdalla – Maelezo
Waziri wa Fedha na Mipango Zanzibar Jamal Kassim Ali ameitaka Bodi ya Mapato zanzibar ZRB kuhakikisha wafanyabiashara wote wanatumia mashine ya utoaji risiti ili kuondosha upotevu wa mapato Nchini.
Hayo ameyasema huko Ukumbi wa Mikutano Wa Bodi ya Mapato Zanzibar ZRB katika kikao kilichojadili kuhusu mfumo mzima wa mashine ya VFMS.
Amesema iwapo wafanya biashara watatumia mashine hiyo ya utoaji risiti kutaondosha mwanya wa upotevu wa mapato kutoka kwa wafanya biashara.
Aidha amesema Serikali inategemea pato lake kutoka kwa wafanya bishara ili kukuza uchumi wa nchi.
“Iwapo wafanya biashara watatumia mfumo wautoaji risiti wa (VFMS) kutaondosha mwanya wa upotevu wa mapato” alisema Waziri Jamal.
Vilevile Waziri huyo ameitaka Bodi ya Mapato Zanzibar kuwasajili wafanya biashara wote wanatumia mashine ya utoaji risiti ili kuwepo kwa usawa kwa wafanya biashara ambao hawatowi risiti na kuondosha malalamiko kwa baadhi yao.
Nae Kamishna wa Bodi ya Mapato Zanzibar ZRB Salum Yussuf Ali amewataka wananchi kuwa na utamaduni wa kudai risiti pale wanaponunua bidhaa kutoka kwa Wafanyabiashara,
Amesema kuwa iwapo mwananchi hatodai risiti kwa mfanya biashaara atakuwa amekwenda kinyume na maagizo ya serikali katika kuikosesha mapato.
Aidha amesema Bodi ya Mapato Zanzibar itahakikisha wafanya biashara wote ifikapo mwishoni mwa mwezi wa Disemba tayari wanatumia mfumo wa utoaji risiti.
Amesema hakutakuwa na msamaha kwa mfanya biashara yoyote Yule ambae hatatumia mashine ya utoaji risti na hatuwa kali zitachukuliwa zidi yake.
Nae mfanyabiashara wa Duka la Saleh Decoration Hassan Saleh Ashuor ameishukuru Serikali kwa jitihada walizochukuwa katika kuwapatia mashine ya utoaji risiti.
Pia amewataka wafanya biashara wenziwe kutumia mfumo huo wa utoaji risiti kwani umekuwa ukirahisha kazi na kuondoa malalamiko kwa waajiri wao.
Waziri jamali alifanya ziara katika maeneo ya Hoteli ya Madinatul-Bahari pamoja na Kampuni ya Saleh Decoretion na kujiridhisha matumizi mazima ya mfumo wa utoaji risiti kwa njia VFMS.