**************************
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ameielekeza Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA kupatia ufumbuzi tatizo la Wizi wa Dawa za Serikali na kutoa onyo kwa Maduka yanayonunua dawa za Wizi.
RC Makalla ametoa maelekezo hayo wakati wa Mafunzo ya siku tano kwa Wakaguzi wa Dawa wa Manispaa za Mkoa huo yaliyolenga kuwajengea uelewa wa maadili ya kazi na utambuzi wa dawa Bandia ili kuongeza ufanisi kwa faida ya watumiaji wa dawa.
Aidha RC Makalla amewataka Wakaguzi wa Dawa kuzingatia Weledi na maadili ya kazi kwa kuhakikisha wanatanguliza uzalendo Kutokana na unyeji wa kazi hiyo ambayo inabeba *dhamana ya Maisha na uhai wa Wananchi.
Hata hivyo RC Makalla ametaka Mamlaka hiyo Kudhibiti tatizo la Vishoka Wanaofanya ziara za ukaguzi kwenye Maduka huku akitaka kuwepo kwa usimamizi madhubuti wa Maduka ya dawa.
Pamoja na hayo RC Makalla ameitaka Mamlaka hiyo kuweka utaratibu wa kufanya ziara za kustukiza kwenye Maduka ya dawa i
=========================
RC MAKALLA APOKEA VIFAA VYA KAMPENI YA USAFI.
– Wadau Wamkabidhi Vifaa vya kufanya Usafi na kuhifadhi taka.
– Waahidi kumpa ushirikiano wa kutosha kuifanya Dar es salaam kuwa Safi.
– RC Makalla Awashukuru wadau na kusema Kampeni hiyo ni endelevu Na siyo nguvu ya Soda.
Kampeni ya usafi iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla imeendelea kuungwa mkono na Wadau mbalimbali ambapo leo kampuni ya GNM Cargo imetoa msaada wa Vifaa vya Usafi ikiwemo Vifaa vya kuhifadhi Usafi Kama sehemu ya kuunga mkono Usafi.
Akipokea Vifaa hivyo RC Makalla amesema ni lazima mandhari ya Jiji la Dar es salaam iwe katika Hali ya Usafi na kupendeza sababu ndio lango la wageni kutoka kila Kona ya Dunia na ndio kitovu Cha Biashara.
Aidha RC Makalla ametoa wito kwa Wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi wa Kampeni ya usafi Disemba 04 kwa kufanya Usafi wa pamoja ambapo Kimkoa Kampeni hiyo itazinduliwa Kata ya Kivukoni.
Aidha RC Makalla ameishukuru kampuni hiyo kwa kuunga mkono kampeni hiyo na kutoa wito kwa wengine kujitokeza.
Kwa upande wake Meneja masoko wa kampuni ya GNM CARGO, Amin Wille Mahava amesema kampuni hiyo itaendelea kutoa ushirikiano kwa RC kwa kutoa vifaa kila mwezi.