Mwanaasha Mtei ambaye ni mnufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) akizungumza na waandishi wa habari waliotembelea katika kijiji cha Rundugai Wilayani Hai kujionea manufaa waliojipatia wanufaika wa mradi huo leo mkoani Kilimanjaro.
Mwanaasha Mtei ambaye ni mnufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) akiwa katika picha ya pamoja na watoto wake wakati waandishi wa habari walipotembelea katika kijiji cha Rundugai Wilayani Hai kujionea manufaa waliojipatia wanufaika wa mradi huo leo mkoani Kilimanjaro.
Haya ni mabaji ya nyumba yake ya udongo iliyoezuliwa na upepo na kuanguka kisha baadaye akaanza kujenga nyumba nyingine mpya kwa matofali ya saruji kwa kuwezeshwa mtaji wa biashara ndi=ogondogo na TASAF.
Mtendaji wa kijiji cha Rundugai Kata ya Mnadani wliaya ya Hai Bw. Descory Mvungi akiwakaribisha waandishi wa habari na maofisa wa TASAF waliotembelea kijiji hicho kwa ajili ya kuzungumza na wanufaika wa mradi huo wa kaya maskini kulia ni Charles Boniface Kodema Mwenyekiti wa kijiji cha Rundugai.
Baadhi ya waandishi wa habari na maofisa wa TASAF waliotembelea katika kijiji hicho wakipata taarifa ya mradi huo kutoka kwa mtendaji wa kijiji Bw. Descory Mvungi.
……………………………………..
Na Mwandishi Wetu
Mwanaasha Mtei ambaye ni mnufaika wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) aliyekuwa anakula mlo mmoja kwa siku baada ya kutelekezwa na mume wake akiwa na watoto sita ameondokana na hali ya utegemezi na kuweza kumsomesha mtoto wake wa kiume Chuo cha Taifa cha Usafirishaji NIT.
Akizungumza Kijiji kwake Rundugai Masana Hai Mkoani Kilimanjaro Mwanaasha amesema, TASAF ilimuwezesha fedha ambazo amezitumia kuanzisha biashara inayomuwezesha kuendesha maisha yake huku akiwahudumia watoto wake.
Akifafanua amesema baada ya maisha kuwa magumu mume wake alimkimbia akiwa na ujauzito ambapo kupitia fedha hizo alianzisha miradi ya ufugaji kuku na mbuzi na kufanya biashara ndogondogo, ambapo kupitia mbuzi ameweza kulipa ada ya mtoto wake Shilingi 800,000 ikiwa ni kwa muhula wa kwanza.
“Kabla ya mradi huu mimi na watoto wangu tulikuwa hatuna hata nguo za kuvaa, nikitaka kutoka ni lazima nikaazime nguo na nikirudi nizirudishe, lakini kupitia fedha za TASAF sasa nina nguo katika kabati langu,” amesema Mwanaasha.
Lakini Mwanaasha sasa amekumbana na janga lingine, nyumba yake aliyokuwa ameijenga kupitia uwezeshaji wa mfuko wa maendeleo ya jamii imekumbwa na upepo mkali na kuanguka, sasa ujenzi wa nyumba nyingi upo katika hatua ya renta na amekwamia hapo kutokana na kutumia fedha zote kwa ajili ya kulipa ada ya mtoto.
Ombi lake kwa mradi huo na wadau wengine ni kumwezesha aweze kumalizia nyumba hiyo ili ahame katika nyumba ya hifadhi anayoishi sasa.
Akizungumzia Mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Hai Dionis Muyinga amesema wametenga zaidi ya Milioni 140 kuwezesha kaya maskini.
Akifafanua amesema baadhi ya kaya ambazo zimewezeshwa zimeshajikwamua na umaskini kwa kujenga nyumba, kuanzisha miradi ya biashara na mifugo inayowaingizia vipato.