Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua kiwanda cha kuongeza thamani zao la mpunga na mazao mbalimbali cha Raphael Group kilichopo Uyole Jijini Mbeya, Novemba 30, 2021. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homela na wa tatu kulia ni Naibu Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kuhusu mazao yaliyohifadhiwa kwenye maghala ya Makampuni ya Raphael Group kutoka kwa Mkurugenzi, Raphael Ndelwa (kushoto) baada ya ufungua kiwanda cha kuongeza thamani zao la mpunga na mazao mbalimbali, eneo la Uyole jijini Mbeya, Novemba 30, 2021. Katikati ni Naibu Spika na Mbunge wa Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Baadhi ya mwananchi wa Mbeya wakimsikiliza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati alipozungumza baada ya kufungua kiwanda cha kuongeza thamani zao la mpunga na mazao mbalimbali cha Raphael Group cha Uyole Jijini Mbeya, Novemba 30, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na Mkurugenzi wa Mkampuni ya Raphael Group, Raphael Ndelwa ( wa pili kulia) baada ya kufungua kiwanda cha kuongeza thamani zao la mpunga na mazao mbalimbali mali ya makampuni hayo eneo la Uyole jijini Mbeya, Novemba 30, 2021. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama kiloba chenye mchele wa kiwango cha daraja la kwanza wakati alipofungua kiwanda cha kuongeza thamani zao la mpunga na mazao mbalimbali cha Makampuni ya Raphael Group eneo la Uyole jijini Mbeya, Novemba 30, 2021. Kulia kwa Waziri Mkuu ni Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson, kulia Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homela na wa pili kulia ni Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Raphael Ndelwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Raphael Ndelwa (kulia) ambye ni Mkurugenzi wa Makampuni ya Raphael Group kuhusu mafuta ya kula yaliyotokana na alizeti yaliyokamuliwa na kufungashwa na makampuni hayo yenye makao makuu Uyole jijini Mbeya, Novemba 30, 2021. Waziri Mkuu alifungua kiwanda cha kuongeza thamani zao la mpunga na mazao mbalimbali cha makampuni hayo. Kushoto ni Naibu Spika na Mbunge wa Mbeya Mjini, Dkt. Tulia Ackson. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)