Kikosi cha KMC FC leo kimeanza rasmi maandalizi kuelekea katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu ya NBC soka Tanzania Bara dhidi ya Geita Gold utakaopigwa siku ya jumapili ya Disemba 5 katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.
KMC FC ambao niwenyeji wa mchezo huo, kikosi kimeanza kujifua mapema leo ikiwa ni baada ya kurejea Jijini Dar es Salaam siku ya Jumapili kutoka Jijini Mbeya ambapo ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Mbeya City uliomalizika kwa sare ya magoli mawili kwa mawili.
Katika maandalizi hayo, Timu hiyo ya Manispaa ya Kinondoni chini ya Kocha Mkuu John Simkoko inakwenda kujiimarisha zaidi ili kuhakikisha kuwa katika mchezo huo ambao itakuwa mwenyeji inabakiza alama tatu muhimu.
KMC FC inahitaji kupata matokeo mazuri katika Uwanja wa nyumbani licha ya kuwa inakutana na Timu ambayo kimsingi ni bora na yenye ushindani lakini maandalizi ambayo yanaenda kufanyika yataleta matokeo chanya.
“Kwenye mchezo wetu uliopita hatujapata kile ambacho tulikuwa tunakihitaji kwa maana ya ushindi, lakini matokeo hayo haya tuvunji moyo badala yake yametupa changamoto ya kuendelea kujiweka vizuri zaidi kwenye mchezo ambao tutakuwa nyunbani.
“Kwetu sisi kama Timu tunahitaji kufanya vizuri kwenye michezo yetu ambayo tunacheza na kwamba bado tunaendelea kupambana ili kufanya vizuri zaidi katika michezo yote iliyopo mbele yetu.