Meneja Mwandamizi wa Chapa ya Coca-Cola Tanzania, Kabula Nshimo (kushoto) akizungumzia juu ya uzinduzi wa kampeni mpya ya ‘Maajabu Halisi na Coca-Cola’ nchini Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Akifuatilia kwa makini kulia ni Meneja Mkuu wa Shughuli za Biashara wa Kampuni ya Coca-Cola, Hellen Masumba. Kampuni itakuwa na wateja kwenye safari ya matukio tofauti ya kusisimua ambayo yatahusisha uzinduzi katika mikoa tofauti kwa lengo la kutambulisha na kuanza kwa kampeni Tanzania kote.
Meneja Mwandamizi wa Chapa ya Coca-Cola Tanzania, Kabula Nshimo (kulia) pamoja na Meneja wa Masoko ya Biashara wa Coca-Cola Kwanza Tanzania, Wahda Mbaraka (kushoto) katika picha ya furaha wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya ‘Maajabu Halisi na Coca-Cola’ kwa mara ya kwanza nchini Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kampuni itakuwa na wateja kwenye safari ya matukio tofauti ya kusisimua ambayo yatahusisha uzinduzi katika mikoa tofauti kwa lengo la kutambulisha na kuanza kwa kampeni Tanzania kote.
Mkurugenzi wa Masuala ya Umma na Mawasiliano wa Coca-Cola Kwanza Tanzania, Salum Nassor, akizungumzia juu ya uzinduzi wa kampeni mpya ya ‘Maajabu Halisi na Coca-Cola’ kwa mara ya kwanza nchini Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kampuni itakuwa na wateja kwenye safari ya matukio tofauti ya kusisimua ambayo yatahusisha uzinduzi katika mikoa tofauti kwa lengo la kutambulisha na kuanza kwa kampeni Tanzania kote
Mtangazaji wa kituo cha luninga cha Clouds TV, Shadee Weris akiwa amepozi kwa furaha wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya ‘Maajabu Halisi na Coca-Cola’ kwa mara ya kwanza nchini Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kampuni itakuwa na wateja kwenye safari ya matukio tofauti ya kusisimua ambayo yatahusisha uzinduzi katika mikoa tofauti kwa lengo la kutambulisha na kuanza kwa kampeni Tanzania kote.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya wa Bongo Flava, Ommy Dimpoz (kulia) akiwa amepozi kwa furaha wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya ‘Maajabu Halisi na Coca-Cola’ kwa mara ya kwanza nchini Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kampuni itakuwa na wateja kwenye safari ya matukio tofauti ya kusisimua ambayo yatahusisha uzinduzi katika mikoa tofauti kwa lengo la kutambulisha na kuanza kwa kampeni Tanzania kote.
Baadhi ya wasanii wa ‘kudensi’ wakiwa wamepozi kwa madaha katika zulia jekundu wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya ‘Maajabu Halisi na Coca-Cola’ kwa mara ya kwanza nchini Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kampuni itakuwa na wateja kwenye safari ya matukio tofauti ya kusisimua ambayo yatahusisha uzinduzi katika mikoa tofauti kwa lengo la kutambulisha na kuanza kwa kampeni Tanzania kote.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya wa Bongo Flava, Rosa Ree (kulia) pamoja na wa ‘kudensi’ Angel Nyigu wakiburudisha kwa mbwembwe wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya ‘Maajabu Halisi na Coca-Cola’ kwa mara ya kwanza nchini Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kampuni itakuwa na wateja kwenye safari ya matukio tofauti ya kusisimua ambayo yatahusisha uzinduzi katika mikoa tofauti kwa lengo la kutambulisha na kuanza kwa kampeni Tanzania kote.
Mtangazaji wa kituo cha redio cha EFM, B Dozen (kulia) akiwa amepozi pamoja na watangazaji wenzake, kutoka kushoto ni Kevoo wa kipindi cha Skonga cha EATV na Idris wa Kitaa wa kipindi cha mashamsham cha Wasafi FM, wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya ‘Maajabu Halisi na Coca-Cola’ kwa mara ya kwanza nchini Tanzania uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Kampuni itakuwa na wateja kwenye safari ya matukio tofauti ya kusisimua ambayo yatahusisha uzinduzi katika mikoa tofauti kwa lengo la kutambulisha na kuanza kwa kampeni Tanzania kote.
…………………………………………………….
Kampuni ya Coca-Cola Tanzania imezindua kampeni mpya inayojulikana kama ‘Maajabu Halisi’, ambayo inamkaribisha kila mtu kusherehekea nyakati tofauti muhimu na za kusisimua kama binadamu.
Kampeni hii inaipa uhai ahadi ya kampuni – ambayo ni kuunganisha na kuwainua watu kila siku – kitu ambacho kinaendana na hali tunayoiishi kwa sasa duniani. Miezi 18 iliyopita ilikuwa na mafunzo mengi: miongoni mwake ni kwamba tunaweza kufurahia kwa pamoja nyakati muhimu tofuati miongoni mwetu pale tunapoungana na kushirikiana katika hali tusiyoitarajia na kutuinua kila siku kwa namna ya kipekee. Lakini pia inatambua changamoto wanazokumbana nazo kizazi cha sasa kutafuta namna bora ya kuishi maisha halisi badala ya kidigitali ambayo kwa asilimia kubwa kimeyazoea.
“Tunapozindua kampeni hii ya ‘Maajabu Halisi’ Tanzania, dhumuni letu kuu ni kuwashirikisha na kusherehekea kwa Pamoja nyakati muhimu na za kusisimua kwenye Maisha yetu tofauti ya kila siku na watumiaji wa bidhaa zetu nchini kote ili kuwainua na kuwaunganisha,” alisema Unguu Sulay, Mkurugenzi Mtendaji, Coca-Cola Kwanza Tanzania.
“Kwa zaidi ya miaka 100, dhima ya Coca-Cola imekuwa ni kusambaza matumaini ambapo kampeni ya ‘Maajabu Halisi’ imekuja kuendeleza ahadi hiyo. Tunaamini kwamba falsafa yake itaendana na watu wote duniani: kwamba wote tunaweza kuwa na nyakati za muhimu na za kusisimua katika Maisha yetu halisi iwapo tutajumuika na kushirikiana kwa Pamoja. Kupitia kampeni hii tutaunganisha na kusherehekea utofauti wa Maisha ya watumiaji wa bidhaa zetu nchini Tanzania kwa kushirikiana na wasanii na wahamasishaji tofauti, kwa lengo la kuwainua na kuwaunganisha watu kwenye nyakati halisi na za kusisimua,” aliongezea Sulay.
‘Maajabu Halisi’ imekuwa kampeni ya kwanza kuzinduliwa na Coca-Cola duniani kote tangu mwaka 2016 ambapo imezinduliwa Pamoja na utambulisho mpya wa Coca-Cola, vilevile na mtazamo mpya kwenye chapa ya Coca-Cola ambayo itahusisha shughuli zote za kimasoko za Coca-Cola. Ikiwa imehamasishwa na kifungashio maarufu cha Coca-Cola, mwonekano wa ‘Kumbato’ ni matokeo ya mabadiliko madogo kwenye chapa iliyozoeleka ambayo yanatoa tafsiri ya kufurahia na kusherehekea nyakati tofauti muhimu na za kusisimua katika shughuli zote za kimawasiliano za Coca-Cola.
Kampeni hii pia itakuwa imebeba kampeni nyingine inayojulikana kama ‘One Coke Away From Each Other,’ ambayo imetengenezwa kwa ajili ya na, jamii inayohitaji kitu tofauti zaidi tofauti na kile ambacho inakitegemea kutoka Coca-Cola. Katika kutengeneza kampeni hii, kampuni imeshirikiana na wasanii, wabunifu, na wahamasishaji wengine tofauti.
Coca-Cola inashirikiana na wasanii, na wahamasishaji mbalimbali kwenye mitandao ya kijamii ili kuipeleka dhana ya ‘Maajabu Halisi’ katika Maisha halisi kupitia chapa yenye muonekano wa ‘kumbato.’ Kupitia utofauti na ubunifu wao, wataweza kuzifanya nyakati za muhimu na kusisimua za kila siku kuwa kwenye uhalisia ambazo ni jumuishi na kuleta umoja, lakini pia zitajipambanua na kuzingatia utofauti.
‘Maajabu Halisi’ si maneno tu ya kawaida au kampeni ya mara moja: ni falsafa na Imani ya muda mrefu ya kampuni ambayo itaziendesha na kuziongoza shughuli za masoko na mawasiliano katika nyote zote za kibiashara za Coca-Cola.
Kampuni itakuwa na wateja kwenye safari ya matukio tofauti ya kusisimua ambayo yatahusisha uzinduzi katika mikoa tofauti kwa lengo la kutambulisha na kuanza kwa kampeni Tanzania kote. Hii itajumuisha kwenye maduka, majumba ya sinema, na maduka makubwa ya manunuzi, kukiwa na ofa kabambe kwa ajili ya wateja. Haya yote yatafikia kilele kwa shamrashamra kadha wa kadha kama vile msafara wa Coca-Cola wa Christmas, kuwepo kwa miti ya Christmas sehemu tofauti za wazi Pamoja na kuzipeleka nyakati za kipekee na kusisimua kwa wasafiri katika mabasi ya umma na kwa wale watakaosafiri kwa treni ili kuwa na wapendwa wao maeneo tofauti ya nchi wakati wa msimu wa sikukuu.
“Kupitia kampeni ya ‘Maajabu Halisi,’ lengo kubwa ni kuwashirikisha watu kwa namna ya kipekee kabisa kupitia matukio tofauti ambayo yatawaacha wakiwa na kumbukumbu nzuri katika Maisha yao. Wateja wetu Tanzania kote watajionea na kushiriki katika shughuli mbalimbali za kusisimua kupitia bidhaa tofauti za Coca-Cola zenye chapa yenye mwonekano unaofanana na ‘kumbato’ kipindi chote cha kampeni. Kuendelea kuwaunganisha watumiaji wa bidahaa zetu na kampeni, tumejipanga kwa shughuli zikiwemo, matukio ya kushtukiza kutoka kwa wasanii na watu maarufu tunaoshirikiana nao ambao watajumuika na wateja katika matukio tofauti miongoni mwa mengi tukayokuwa tukiyafanya,” alisema Kabula Nshimo, Meneja Mwandamizi wa Coca-Cola Tanzania.