WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso katikati akitoa tuzo kwa mmoja wa wawakilishi wa Kijiji bora Kimanga wilayani Pangani Mkoani Tanga vilivyofanya vizuri kwenye mapambano ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
WAZIRI wa Maji na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso katikati akizinduzi wa Igizo la Radio lenye lengo la kuyawezesha makundi ya waendesha pikipiki maarufu Bodaboda kushiriki kwenye mapambano ya ukatili dhidi ya wanawake, watoto na wenza.
WAZIRI wa Maji na Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) Jumaa Aweso akizungumza wakati wa halfa hiyo
MKUU wa wilaya ya Pangani Ghalibu Ringo akizungumza wakati wa halfa hiyo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Pangani Akida Bohorera akizungumza
Mkurugenzi wa Uzikwasa Novatus Urassa akizungumza wakati wa halfa hiyo
Mwakilishi Hakimu Mkazi Mfawidhi ,Hakimu Mkazi wa Mahakama ya wilaya ya Pangani Fransisca Magwiza
Mwakilishi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa wilayani Pangani (Takururu) akizungumza
Wasanii wilayani Pangani wakitoa burudani
****************************
OSCAR ASSENGA, PANGANI.
WAZIRI wa Maji Jumaa Aweso amesema kasi ya mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia wilayani Pangani yanatakiwa kuongezwa nguvu kwa sababu hawataki kusikia vitendo vya ubakaji na ulawiti vikiendelea.
Aweso ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Pangani (CCM) aliyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Igizo la Radio lenye lengo la kuyawezesha makundi ya waendesha pikipiki maarufu Bodaboda kushiriki kwenye mapambano ya ukatili dhidi ya wanawake, watoto na wenza.
Igizo lilikwenda sambamba na Kampeni ya Mapambano dhidi ya vitendo vya unyanyasaji wa jinsia lilioandaliwa na Shirika la Uzikwasa lenye makazi yake wilayani Pangani Mkoani Tanga ikiwemo kutoa zawadi kwa vijiji bora vilivyofanya vizuri kwenye mapambano ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Alisema hawataki kusikia watu wanabakwa huku akilitaka Shirika la Uzikwasa watoke na kwenda kuwaelimisha fursa zinazowazunguka wilaya ya Pangani kutokana na uwepo wa maji yanayotiririka baharini wakati hawana hata shamba la kulimia mchicha.
“Ndugu yangu Akida wewe ni Mwenyekiti wa Halmashauri tutakuwa wasaliti wakubwa kama hatutakuwa tumetenda haki kwa wananchi kama tutakuwa sehemu ya kuwapigia Maocd mahakami kwamba aliyefanya tukio hilo ni mwenzetu tumsamehe”Alisema Waziri Aweso
Alisema yeye hawakuwa tayari ya kuwaombea msahama watu wanaofanya vitendo vya namna hiyo badala yake nitahakikisha wanachukuliwa hatua kali za kisheria ili kuweza kudhibiti vitendo hivyo kwa jamii.
“Uchungu wa u mwana aujuaye ni mzazi hebu fikiria wewe mama umezaa mtoto wa kiume ambaye atakuja kusaidia jamii yake anashindwa kufikia malengo kwa sababu ameharibiwa hii sio sawa kabisa lazima tuchukue hatua “Alisema
“Wakati mwengine unasikia mtu anabakwa mpaka anafikia hatua ya kufa na kushindwa kufikia malengo yake nani aje aseme hapo niwaombe wazazi wangu na wananchi mtu yoyote ambaye atataka kutuharibia jamii yetu ya Pangani lazima tumnyooshee vidole na achukuliwa hatua tunasema uzikwasa tupo tayari kushirikiana nanyi”Alisema
Awali akizungumza wakati wa tamasha hilo Mkuu wa wilaya ya Pangani Ghaibu Lingo alisema ukatili wa kijinsia kwa sisi watu wa Pangani wazazi ndio wanaanza kwa kuwakatili watoto na wakina mama.
Alisema wamewakatili wakiiamini kuwa ni tamaduni waziache huku akieleza kwamba sasa ameanzisha taratibu kwamba taarifa ya ukatili ikikingia kwenye mikono yake akisikia imefika mahakamani na watu hawajaenda kutoa ushahidi atawashughulikia.
“Kwa sababu haiweziekani mtu ameharibika na unashindwa kutoa ushaidi mahakamani na ndio maana ukatili unaongezeka sasa kama DC ndio mimi mwenyewe nikisikia taarifa ya ukatili na mtu akijaribu kuiharibu walahi tutawashughulikia”Alisema
Naye kwa upande wake Mwenyekiti Halmashauri Akida Bahorera alilipongeza Shirika la Uzikwasa kwa jinsi wanavyofanya kazi nzuri na kubwa ya kutoa elimu ya kupambana na ukatili wa kijinsia.
Alisema wanafanya kazi kubwa ya kuelimisha wakina mama wamepata elimu kubwa ya kupambana na ukati wa kijinsia na wamewaunganisha wana vijiji na matunda yake yameonakana kwani ripoti inayotolewa na vijiji kuita vikao na kusaidia maendelea ya jamii.
Hata hivyo alisema Shirika la Uzikwasa limetusaidia kwenye eneo la mguso maana yake watu wa bodaboda wakati hawajapata elimu ilikuwa ni eneo hatarishi kwa vijana lakini kutokana na elimu hiyo imewabadilisha na kuondokana na vitendo hivyo huku akieleza halamshauri haitutakuwa vikwazo badala yake watashirikiana nayo.