Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Jamal Kassim Ali akifungua Mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wahasibu wa Serikali juu ya matumizi ya Mfumo wa ukusanyaji mapato kwa njia ya Kielektoniki ZanMalipo (GePG) mafunzo yaliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Shirika la Bima, Mpirani Zanzibar.
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo ya siku tatu ya kuwajengea uwezo wahasibu wa Serikali juu ya matumizi ya mfumo wa ukusanyaji mapato kwa njia ya Kielektoniki ZanMalipo (GePG) wakisikiliza hutuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Fedha na Mipango Jamal Kassim Ali (hayupo pichani).
Afisa Tehama Muandamizi kutoka Wizara ya Fedha Tanzania Bara na Mkuu wa Mfumo wa GePG Basil S. Baligumya akielezea juu ya umuhimu wa mafunzo ya ukusanyaji mapato katika hafla ya mafuzo ya siku tatu iliyofanyika ukumbi wa mikutano wa Shirika la Bima, Mpirani Mjini Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji Wakala wa Serikali Mtandao Zanzibar Said Seif Said akizungumza na wandishi wa habari kuhusu zamira yao ya kuwaezesha wahasibu wa Serikali kujua namna ya kutumia mfumo wa kielektoniki wa ukusanyaji mapato.
Picha na Makame Mshenga.