VINARA, Chelsea wamepunguzwa kasi baada ya sare ya 1-1 na Manchester United katika mchezo wa Ligi Kuu ya England Uwanja wa Stamford Bridge Jijini London.
Jadon Sancho alianza kuifungia Manchester United dakika ya 50 hilo likiwa bao lake la pili wiki hii, kabla ya Jorginho kuisawazishia The Blues kwa penalti dakika ya 69 kufuatia Aaron Wan-Bissaka kumchezea rafu Thiago Silva.
Chelsea inafikisha pointi 30 baada ya sare hiyo na kuendelea kuongoza Ligi kwa pointi mbili zaidi ya Manchester City, wakati Man United inafikisha pointi 18 katika nafasi ya nane baada ya timu zote kucheza mechi 13.