*********************
NJOMBE
Ili Kukabiliana na Changamoto ya Usafiri Kwa ajili ya Ufuatiliaji wa Miradi Mbalimbali Inayotekelezwa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Imelazimika Kutumia Kiasi Cha Zaidi ya Shilingi Milioni 80 Kununua Gari Aina ya Ford Ranger Ili Kupunguza Changamoto Hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa Kasongwa Ametoa Taarifa ya Ununuzi wa Gari Hilo Mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe wakati akizindua Maonyesho ya Miaka 60 ya Uhuru ya Kimkoa Yanayofanyika Stendi ya Zamani Mjini Njombe.
“Mheshimiwa mkuu wa mkoa tunaomba utukabidhi gari aina ya Ford Ranger ambayo halmashauri ya wilaya ya Njombe kununua gari kwa kutumia mapato ya ndani na tunaikabidhi kwa mhandisi aliyeletwa hivi karibuni ,anasema mkuu wa wilaya ya Njombe Kissa Gwakisa “Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Bi.Sharifa Nabarang’anya Amesema Gari Hilo Lililonunuliwa Kupitia Fedha za Mapato ya Ndani Kwa Sasa Litatumika Zaidi Katika Miradi ya Ujenzi Ili Kukabiliana na Kasi ya Serikali ya Kutaka Miradi Mingi Itekelezwe Kwa Wakati.
“Tulikuwa na changamoto kubwa ya magari kwahiyo tumenunua ili lisaidie kufanya ufatiliaji na usimamizi wa miradi ya halmashauri ,Anasema mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Sharifa Nabarang’anya “
Baada ya Kuzindua Maonyesho Hayo Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhandisi Marwa Rubirya Pia Amekabidhi Gari Hilo Kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe na Kuagiza Likafanye Kazi Iliyokusudiwa.
“Nakabidhi gari hii ambayo ni mpya na itumike kwa kazi iliyokusudiwa ,Anasema mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya “
Erasto Ngole ni Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Mkoa wa Njombe Ambaye Amekiri Kuwapo Kwa Kasi Kubwa ya Maendeleo Yanayopigwa Chini ya Usimamizi wa Mkuu wa Mkoa na Wasaidizi Wake.