Taasisi ya Miriam Odemba wakikabidhi msaada watoto wenye mahitaji maalum wakati wa utoaji wa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto wenye mahitaji maalum wa kituo cha Salvation Army kilichopo Temeke. Baadhi ya Watumishi wa Taasisi ya Miriam Odemba wakipata chakula pamoja na watoto wenye mahitaji maalum wakati wa utoaji wa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto wenye mahitaji maalum wa kituo cha Salvation Army kilichopo Temeke. Mwanamitindo maarufu hapa nchini Bi.Miriam Odemba akipata chakula cha pamojja na watoto weenye mahitaji maalumu wakati wa utoaji wa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto wenye mahitaji maalum wa kituo cha Salvation Army kilichopo Temeke.
Mwanamitindo maarufu hapa nchini Bi.Miriam Odemba akizungumza na baadhi ya watoto wenye ulemavu wakati wa utoaji wa msaada wa vitu mbalimbali uliombatana na kupata chakula cha pamoja na watoto wenye mahitaji maalum wa kituo cha Salvation Army kilichopo Temeke.
*****************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Watanzania wametakiwa kujitokeza kuwasaidia watoto wenye Mahitaji Maamlumu wakiwemo yatima na wasiokuwa na walezi kuliko na siyo kujikita kuchangia mambo ya starehe pekee.
Rai hiyo imetolewa jijini Dar es salaam,na Mwanamitindo maarufu hapa nchini Bi.Miriam Odemba wakati wa utoaji wa msaada wa vitu mbalimbali uliombatana na kupata chakula cha pamoja na watoto wenye mahitaji maalum wa kituo cha Salvation Army kilichopo Temeke.
Mwanamitindo huyu amesema kuwa watanzania wamekuwa nyuma kwenye masuala ya kusaidia jamii lakini kwenye shughuli za kuchangia maharusi na sherehe mbalimbali wamekuwa wakijitokeza jambo ambalo wakati mwingine halina tija kwa jamii.
Aidha amewataka warembo na wanamitindo wengine kuungana naye kuwawezesha wenye mahitaji maalum ili kuweza kutokomeza umasikini unawasumbua watoto hao katika maeneo mbalimbali.
Odemba amewaomba wafadhili wengine nchini na nje ya nchi kujitokeza kuwaunga mkono taasisi hiyo kwa kuwapa masaada ili kuendelea kusaidia watu wenye mahitaji maalum
Kwa upande wake Msimamizi Mkuu wa kituo cha Salvation Army Bw. George Mbegani Mwasenga amesema kuwa ujio wa taasisi ya Miriamu Odemba imekuwa faraja kubwa kwa watoto hao wenye mahitaji maalum na kuwaomba watanzania wengine kujitokeza kwenda kuwatazama.
Aidha amesema kuwa kituo hicho kinakabiliwa na changamoto kadhaa ikiwemo Kuwama kwa baadhi ya mambo ambayo ni mahitaji maalum kwa watoto hao kutokana na gharama kuwa kubwa ikiwemo
Ameishukuru taasisi ya Mariam Odemba kuwa sehemu ya faraja yao kwa kujitokeza kuwatembelea na kula nao pamoja na kuwapatia zawadi mbalimbali.