………………………………………………………..
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh.Anthony Mavunde jana amezindua rasmi Umoja wa Familia ya Wanamichezo wa zamani Dodoma (UFAWAZA) na kupewa heshima ya kuwa mwanachama wa kwanza wa heshima.
Uzinduzi huo ulifanyika jana katika Hotel ya Royal Village Dodoma na kuhudhuriwa na wanamichezo mbalimbali wa zamani ambao Mbunge Mavunde amejitolea kuwalipia bima ya jamii kwa miaka miwili itakayogharimu5 Tsh 4,000,000 kupitia benki ya Biashara Tanzania (TCB) ambayo zamani ilitambulika kama benki ya Posta.
“Nawashukuru wazee wangu kwa kunipa heshima hii kubwa ya kuwa mmoja wa wanafamilia na kuwa mwanachama wa kwanza wa heshima wa UFAWAZA.
Nawapongeza kwa kuja na wazo hili la kuunda umoja huu wa kuwakutanisha wachezaji wa zamani wa Dodoma,ambao pia mtasaidiana katika shida na raha.
Huwa najisikia vibaya sana kuona wachezaji wengi wa zamani wakipata changamoto za matibabu kwa ukosefu wa fedha na kupelekea umauti wao,naamini kwa huduma ya BIMA JAMII itakuwa imesaidia sana kuwaondolea mzigo mkubwa wanamichezo ,na mimi nitawalipia wanachama wote 75 wa awali bima ya jamii kwa miaka miwili”Alisema Mavunde
Akizungumza kwa niaba,Mwenyekiti wa UFAWAZA DODOMA Ndg. Ally Kheri amemshukuru Mbunge Mavunde kwa namna alivyowakimbilia na kuwashika mkono tangu kuanzishwa kwa umoja huo na kuahidi kuuboresha umoja huo ili malengo ya uanzishwaji wake yaweze kutimia.