Kaimu Mkurugenzi Idara ya Miliki TBA,Bw.Said Mndeme,akizungumza na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),Joseph Kilangi pamoja na watumishi wa Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA) ambao walifanya ziara ya kujifunza na kujionea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA) Mhandisi Kassim Omar,akielezea jambo wakati wa ya kujifunza na kujionea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),Joseph Kilangi (aliyevaa miwani) akimsikiliza Mhandisi ujenzi katika eneo la Viwanda vya Tofali na Zege Athu Chulla akitoa maelezo ya mradi katika eneo la Nzuguni wakati wa ziara ya kujifunza na kujionea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),Joseph Kilangi (aliyevaa miwani) akifafanua jambo wakati wa ziara ya kujifunza na kujionea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
Mratibu wa ujenzi wa nyumba 3,500 Nzugani Dodoma (Awamu ya kwanza nyumba 150) Fedrick Jackson,akimpa maelezo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),Joseph Kilangi (aliyevaa miwani) pamoja watumishi wa wakala wa majengo Zanzibar (ZBA) wakati wa ziara ya kujifunza na kujionea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
Ujenzi wa nyumba 150 katika eneo la Nzuguni ukiendelea
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),Joseph Kilangi akiangalia ujenzi wa mradi katika Mji wa Kiserikali Mtumba wakati wa ziara ya kujifunza na kujionea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),Joseph Kilangi,(aliyevaa miwani) akitoa maelezo mara baada ya kukagua ujenzi wa nyumba 20 zilizopo katika eneo la Kisasa wakati wa ziara ya kujifunza na kujionea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),Joseph Kilangi ,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufanya ziara ya kukagua,kujifunza na kujionea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Miliki TBA,Bw.Said Mndeme,akimpongeza Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),Joseph Kilangi kwa kutembelea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA) Mhandisi Kassim Omar,akielezea jinsi walivyojifunza katika ziara ya kukagua miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Idara ya ujenzi TBA,Mhandisi Likimaitare Naunga,akiwaahidi ushirikiano viongozi wa ZBA katika kutekeleza miradi mbalimbali nchini pamoja na kubadilishana uzoefu wa kazi.
…………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ),Joseph Kilangi amesema mpango uliopo kwa sasa ni Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kushirikiana na Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA) katika kutekeleza miradi mbalimbali visiwani Zanzibar.
Pia wameridhishwa na miradi inayotekelezwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambapo kupitia Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA) wameahidi kufanya miradi yenye kiwango kama hicho visiwani Zanzibar.
Kauli hiyo ameitoa leo Novemba 26,2021 wakati wa ziara ya Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA) kujifunza na kujionea miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na TBA Jijini Dodoma.
Miradi hiyo ni pamoja na ule wa Mji wa Kiserikali Mtumba awamu ya pili,mradi wa ujenzi wa nyumba 3500 wa watumishi wa umma,Nzuguni ambao umeanza na nyumba 150 na mradi wa ujenzi wa nyumba 20 za viongozi katika eneo la Kisasa.
Katibu Mkuu Kilangi amesema kwa sasa wanaiamini TBA kwa asilimia mia moja hivyo watashirikiana na ZBA kutekeleza miradi mbalimbali visiwani Zanzibar kwa lengo la kupata miradi yenye ubora kama Tanzania Bara.
“Sasa mimi nadhani tuiamini TBA kwa asilimia miamoja kama tunamiradi tutakayoianzisha basi TBA na wana miradi Zanzibar tutawaleta wataalamu wetu waje wafanye kazi kwa pamoja na TBA.
“Wanzanzibar wategemee tutawaalika TBA Zanzibar, wategemee mambo mazuri hizi fedha tulizopata tuna bilioni 460 zinaenda mifukoni mwa watu kupitia miradi mbalimbali.Tutawambia waje Zazibar wasimamie miradi yetu,”amesema.
Aidha,amesema mradi wa Mji wa Serikali awamu ya pili ni mzuri na utaonesha kwamba Dodoma ni Makao Makuu ya Serikali kama ilivyo Lagos na ndoto ya Hayati mwalimu Julius Kambarage Nyerere itakuwa imetimia kwa vitendo.
“Mradi ule wa Mji wa Serikali ni mzuri sana na majengo yale hasa awamu ya pili ikikamilika mji utakuwa ni mzuri sana lakini itaonesha kwamba hapa ni Makao Mkuu ya Nchi hata ukienda Lagos utaona hili nadhani ile ndoto ya Baba wa Taifa itatimia.
“TBA wamekuja na michoro mizuri na inajengwa kileo sana mazingira ni mazuri na vitendea kazi vimezingatia ubora,baada ya miaka miwili mitatu itaonekana kweli ni makao makuu ya Serikali,”amesema.
Kuhusiana na nyumba za watumishi wa umma zinazojengwa na TBA, amesema mradi huo utakuwa na manufaa makubwa kwani watumishi wataweza kukaa katika nyumba nzuri.
Hata hivyo ameipongeza TBA kwa kufanya kazi nzuri ikiwa ni pamoja na kuwa na vifaa pamoja na wataalamu wa kutosha.
“Mimi kwa TBA kwakweli kwa uwezo nilioouna mimi nadhani hata kama kuna wakandarasi wengine kuna miradi mbalimbali ya ujenzi ni kushawishi tu waitumie TBA kama ni Mkandarasi waitumie TBA kama ni msimamizi kwa sababu wana uwezo wote wana vifaa wana zana na wana wataalamu wa kutosha,”amesema.
Kwa upande wake,Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Majengo Zanzibar (ZBA) Mhandisi Kassim Omar amesema lengo la ziara hiyo ni kujifunza yale ambayo TBA wanayafanya ambapo kwa kiwango kikubwa yanalingana na majukumu ya ZBA.
”Zanzibar kwa sasa wapo katika matayarisho ya Mji wa Kiserikali visiwani humo ambapo utekelezaji wao utakuwa ni mkubwa ambapo amewakaribisha TBA waone yale ambayo wameyaonesha tutakavyoyatekeleza.”amesema Mhandisi Omar
Naye,Kaimu Mkurugenzi Idara ya Miliki TBA,Bw.Said Mndeme amesema ziara hiyo imekuwa na manufaa makubwa kwani ZBA wameweza kuona mradi wa nyumba za watumishi wa umma na wameona jinsi walivyoutekeleza mradi huo na wameweza kujionea jinsi ambavyo wamejipanga katika eneo la material pamoja na viwanda mbalimbali ambavyo wamevianzisha.
Kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya ujenzi TBA,Mhandisi Likimaitare Naunga ameishukuru ZBA kwa kuichagua TBA kama sehemu ya kupata uzoefu katika sekta ya ujenzi ambapo amedai wapo tayari kwa ajili ya ushirikiano huo.