Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti wa dawa na vifaa tiba (TMDA) Bw. Adam Fimbo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuhusu utekelezaji wa mradi wa kujenga mifumo imara na thabiti ya udhibiti ya kufanya utafiti wa majaribio ya dawa.Mkurugenzi wa Utafiti katika kituo cha Kilimanjaro Clinical Research Institute (KCRI) Profesa Blandina Theophil Mbaga akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa mradi wa kujenga mifumo imara na thabiti ya udhibiti ya kufanya utafiti wa majaribio ya dawa.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa kujadili utekelezaji wa mradi wa kujenga mifumo imara na thabiti ya udhibiti ya kufanya utafiti wa majaribio ya dawa. Washiriki wa mkutano wa kujadili utekelezaji wa mradi wa kujenga mifumo imara na thabiti ya udhibiti ya kufanya utafiti wa majaribio ya dawa akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti wa dawa na vifaa tiba (TMDA) Bw. Adam Fimbo wakiwa katika picha ya pamoja.
*******************.
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM
Mamlaka ya udhibiti wa dawa na vifaa tiba (TMDA) wamekutana na wadau mbalimbali wanaohusika katika utekelezaji wa mradi wa kujenga mifumo imara na thabiti ya udhibiti wa kufanya utafiti wa majaribio ya dawa jambo ambalo litasaidia wanaofanya utafiti kufanya kwa mujibu wa taratibu uliowekwa.
Mradi huo ni wa miaka miwili na nusu ulianza kutekelezwa mwaka wa jana chini ya ufadhili, ambapo aasisi mbalimbali zinazohusika wamekutana kwa ajili ya kujadili maendeleo ya maradi ili kuhakikisha unaendelea kufanyika kwa ufanisi ili kuwalinda watu wanaoshiriki katika majaribio ya dawa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya udhibiti wa dawa na vifaa tiba (TMDA) Bw. Adam Fimbo, amesema kuwa wamepokea fedha kutoka kwa wafadhili kwa ajili ya kufanya miradi mbalimbali inayolenga kujenga mifumo imara na thabiti ya udhibiti wa bidhaa kwa mujibu wa sheria.
Bw. Fimbo amesema kuwa mradi huo utasaidia kuweka muongozo mizuri inayofanana, kufanya mafunzo kwa watalaamu katika masuala ya kupitisha majaribio ya dawa nchini kwa ajili ya kuwalinda watu wanaoshiriki katika majaribio.
“Kupitia mradi huu umesaidia kuweka mifumo thabiti kwa ajili ya majaribio, masuala ya ufatiliaji na usalama kwa sababu ukitoa dawa ya majaribio haujui kama zina madhara kwa watu au hapana, katika sekta ya dawa hauwezi kumruhusu mtu atumie mpaka ifanyiwe majaribio ikianzia kwa wafanyama na baadaye kwa binadamu” amesema Bw. Fimbo.
Bw. Fimbo amesema kama sehemu ya utekelezaji ya sheria ya dawa na vifaa tiba sura ya 219 wana uwajibu wa kuweka mifumo ya udhibiti masuala ya majaribio ya dawa.
“Tuna jukumu la kudhibiti taratibu za tafiti, jinsi ya kutoa dawa kwa binadamu, nini kifatwe, taarifa gani za msingi ziwasilishwe, maeneo gani ya majaribio yanatakiwa kufanyika” amesema Bw. Fimbo.
Mkurugenzi wa Utafiti katika kituo cha Kilimanjaro Clinical Research Institute (KCRI) Profesa Blandina Theophil Mbaga, amesema kuwa wao ni sehemu ya watu wanaoshiriki katika mradi huo.
Prof. Mbaga amesema kuwa wakiwa kama wadau katika masula ya utafiti wanaendelea kuhakikisha wanatekeleza mradi huo kwa ufanisi.