Mkurugenzi wa masoko na huduma kwa wateja shirika la bima la Taifa (NIC) , Yessaya Mwakifulefule akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha.
Mkurugenzi wa masoko na huduma kwa wateja shirika la bima la Taifa (NIC) Yessaya Mwakifulefule akitoa maelekezo kwa baadhi ya wafanyakazi wake katika banda lao katika uwanja wa Stadium jijini Arusha.
……………………………………………………………
Happy Lazaro, Arusha
Arusha.SHIRIKA la Bima la Taifa, (NIC), limewataka Watanzania waendeshaji wa vyombo vya moto na watumiaji wa barabara kutii sheria bila shuruti ili kuepuka ajali zisizo za lazima.
Mkurugenzi wa Masoko na huduma kwa wateja wa shirika hilo, Yessaya Mwakifulefule ameyasema wakati akiongea na japo la waandishi wa habari kuhusiana na huduma wanazotoa .
Kwa upande wake Meneja wa bima Mkoa wa Arusha John Mdenye amesema wiki hiyo ya nenda kwa usalama watawafikia wateja mbali mbali kuwapa mafunzo juu ya umuhimu wa wa kukata bima katika vyombo.
Amesema kuwa, wananchi wengi wamekuwa na tabia ya kutokukata bima mpaka pale wanapopata matatizo ya majanga ya Moto ndio wana ona umuhimu wa kukata bima ya vyombo vya moto hivyo kutumia wiki hiyo kikamilifu kufikisha ujumbe wa umuhimu wa bima .
Naye Afisa bima Constancia Komanya amesema wataendesha mafunzo kwa vijana wanao miliki vyombo vya moto ikiwemo piki piki, dala dala na wenye magari ya tax watafuatwa katika vijiwe vyao na kupewa mafunzo ya umuhimu wa ukataji wa bima.
Amesema kuwa,watawaeleza wamiliki wa vyombo vya moto faida na hasara za kuwa na bima na nini cha kufanya waweze kujikinga na majanga yanayo tokea katika vyombo vya moto na vile wanavyo miliki majumbani mwao.