…………………………………………………………..
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya kwa kushirikiana na Polisi Mkoa wa Songwe kuanzia tarehe 22/11/2021 hadi 23/11/2021 lilifanya misako katika maeneo mbalimbali ya Mji Mdogo wa Tunduma mkoani Songwe na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa watano [05] mtandao wa wezi wa Pikipiki.
Watuhumiwa waliokamatwa ni:- 1. DAUD MTAMBO @ KENSON [26] Mkazi wa Tunduma, 2. MAJALIWA MKONDYA [32] Mkazi wa Tunduma, 3. JUMANNE ANTHONY [46] Mkazi wa Mpemba – Tunduma, 4. CLAUD MSAFIRI @ SILUNGWE [31] Mkazi Sogea – Tunduma na 5. NICHOLAUS NJEJE [36] Mkazi wa Laela – Sumbawanga.
Watuhumiwa ni wanunuzi, wauzaji, wabadilishaji muonekano na wezi wa Pikipiki katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Mbeya na Songwe. Watuhumiwa ni mtandao mmoja na watuhumiwa waliokamatwa tarehe 21.11.2021 majira ya saa 11:30 alfajiri huko katika Msitu wa Hifadhi ya Mbiwe, Kata ya Makongolosi, Tarafa ya Kiwanja, Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya ambao ni 1. MUGANYIZI VICTOR LEOPORD [36] mkazi wa Ngokolo na 2. MAJALIWA MWASHUYA [31] mkazi wa Sogea – Tunduma ambao walikamatwa wakiwa na Pikipiki ya wizi Na. MC.810 CCH Kinglion mali ya GODLUCK ANDENGULILE [22] Mchimbaji na Mkazi wa Matundasi.
Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
WAWILI WATIWA MBARONI KWA TUHUMA YA MAUAJI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili 1. GAIDON NDIMBO [31] Askari Idara ya Uhamiaji Wilaya ya Mbeya na Mkazi wa Ilomba na 2. BIDI MWAKWINYA [29] Mkazi wa Mabatini Jijini Mbeya kwa tuhuma za mauaji ya FRANCIS CHRISTOPHER [23] Mkazi wa Mabatini.
Ni kwamba mnamo tarehe 22.11.2021 majira ya saa 02:00 usiku huko maeneo ya Chuo Kikuu cha Mzumbe Tawi la Mbeya kilichopo mtaa wa Forest ya zamani FRANCIS CHRISTOPHER alikamatwa na kushambuliwa na watuhumiwa kutokana na tuhuma za wizi wa simu ya mkononi.
Watuhumiwa baada ya tukio hilo, walimfikisha kituoni FRANCIS CHRISTOPHER akiwa katika hali mbaya na alipopelekwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya kwa ajili ya matibabu alifariki dunia. Upelelezi wa shauri hili unaendelea na mara baada ya kukamilika watuhumiwa watafikishwa mahakamani.
KUPATIKANA NA POMBE MOSHI @ GONGO.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia EDA LYAMBA [66] Mkazi wa Airport ya Zamani Jijini Mbeya akiwa na lita tatu za Pombe haramu ya Moshi @ Gongo.
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 23.11.2021 majira ya saa 05:00 asubuhi katika msako uliofanyika maeneo ya Airport ya Zamani, Kata ya Iyela, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya. Mtuhumiwa ni muuzaji wa Pombe hiyo.
KUPATIKANA NA KARATASI ZA KUTENGENEZEA NOTI BANDIA.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia JACKSON STANTANIA [23] Mkazi wa Airport ya zamani akiwa na karatasi za kutengenezea noti bandia.
Mtuhumiwa alikamatwa mnamo tarehe 23.11.2021 majira ya saa 06:00 mchana huko maeneo ya Ituha, Kata ya Ilomba, Tarafa ya Iyunga, Jijini Mbeya katika misako inayoendelea katika maeneo mbalimbali ya Jiji na Mkoa wa Mbeya.
Imetolewa na:
[ULRICH O. MATEI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.