WAZIRI wa Madini Doto Biteko akizungumza na wachimbaji wadogo wa madini waliopo Mgodi wa Seita uliopo Kijiji cha Chamtui Kata ya Kikunde wilayani Kilindi mkoani Tanga wakati wa ziara yake ya siku moja |
Mkuu wa wilaya ya Kilindi Abel Busalama akizungumza wakati wa ziara hiyo kulia ni Afisa Madini Mkazi wa Mkoa wa Tanga Zabibu Napacho na kushoto ni Waziri wa Madini Dotto Biteko |
MBUNGE wa Jimbo la Kilindi (CCM) Omari Kigua akizungumza wakati wa ziara hiyo |
Shemeu ya wananchi wakimsikiliza kwa umakini Waziri wa Madini Doto Biteko
WANANCHI wakimsikiliza Waziri wa Madini Dotto Biteko ambaye hayupo pichani |
WAZIRI wa Madini Doto Biteko katika akiwa na Mkuu wa wilaya ya Kilindi Abel Busalama na kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Kilindi (CCM) Omari Kigua
NA OSCAR ASSENGA,KILINDI
WAZIRI wa Madini Doto Biteko ametoa wito kwa wachimbaji wadogo wa madini waliopo Mgodi wa Seita uliopo Kijiji cha Chamtui Kata ya Kikunde wilayani Kilindi mkoani Tanga kutokubali madini wanayochimbwa yatoroshwe badala yake wayasimamie vizuri ikiwemo kufuata sheria zilizowekwa.
Biteko aliyasema hayo leo wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani Kilindi ambapo alikwenda kutembelea wachimbaji wadogo kwenye mgodi wa huo ambapo alisema kila dhahau inayopatikana ipelekwe kwenye soko iuzwe na yoyote anayeuza nje ya soka unavunja sheria.
Waziri Biteko alisema hivi sasa wanakamilisha utaratibu baada ya kituo cha kuuzia madini kufika kwenye eneo hilo hakuna dhahabu hata gramu moja itakayotoka nje ya wilaya ya Kilindi ili Halmashauri iweze kupata mapato.
“Baada ya kituo cha Kuuza Madini kufika hapa hakuna dhahabu hata gramu moja itakayotoka nje ya wilaya ya Kilindi kwani kufanya hivyo kutawezesha halmashauri iweze kupata mapato na seriukali kuu ipate mapato”Alisema
“Kwani kuna watu wanabeba dhahabu kwenda Dar es Salaam wakienda huku anawanaweza kupoteza hiyo dhahabu isionekane tunaweka huu utaratibu tumekubaliana na DC “Alisema Waziri Biteko.
Aidha pia Waziri huyo alimuagiza Mkuu wa wilaya ya Kilindi Mkoani Tanga Abel Busalama kuhakikisha ndani ya wiki moja wanaanzisha kituo cha Kuuzia Madini kwenye Mgodi Kijiji cha Seita Kata ya Kikunde badala ya kuwa na soko eneo la mjini ambako hakuna dhahabu.
Alisema na wapo wanunuzi wengine wanakuwa na ule utaratibu wa kwenda kwenye mashimo huku akieleza huo utaratibu haupo badala yake wanapaswa kufika katika soko la dhahabu.
“Kwani kwenda kwenye mashimo, mialo ndio watakuwa wanachochea utoroshaji wa madini tunakubalina kituo kitakuwepo hapo na bei ya madini kila siku itabandikwa ukutani na na tume ya Madini.
Hata hivyo alisema eneo hilo watapeleka Afisa wa kukaa hapo hapo ili aweze kusimamia mambo mengine ikiwemo kuondosha changamoto ambazo zimekuwa zikijitokeza .
Awali akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkuu wa wilaya ya Kilindi Abel Busalama alisema wilaya hiyo haijanufaika na ipasavyo na uwepo wa madini kutokana na kukosekana kwa soko la kuuzia.
Alisema hatua hiyo inasababisha wachimbaji waliopo wilayani humo kulazimika kwenda kuuza madini yao wilaya jirani na hivyo kukosa mapato Halmashauri na kuchochea utoroshaji wa madini.
Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa Wachimbaji wa wadogo wadogo katika eneo la Mgodi Seita Luandamilo, Fransis Mgasa alisema wana luandamilo wanafanya kazi kwenye leseni ya Chapakazi Group yenye leseni nne na zinaishia mahali fulani na maduara mwengine hayapo kwenye leseni.
Alisema wanamuomba Waziri huyo awasaidie wachimbaji hao wadogo eneo ambalo wanachimba sasa ambazo hazipo ndani leseni hizo nne za chapakazi.