Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimshuhudia Mkewe Mama Mary Majaliwa (kulia) akimkabidhi Nahodha wa timu ya Mbekenyera Queens, Saada Aucho zawadi ya Sh. milioni 2, jezi na mpira baada ya timu hiyo kuibuka na ubingwa wa kombe la jimbo la Rungwa kwenye uwanja wa Shule ya Wonder Kids Ruangwa, Novemba 22, 2021. Mbekenyera Queens waliibuka na ushind wa penati 3-1.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary wakiwa katika picha ya pamoja na mabingwa wa Michuano ya Kombe la Jimbo la Ruangwa kwa wanawake, Mbekenyera Queens baada ya timu hiyo kuifunga Mandawa Queens kwa penati 3-1 katika mchezo wa fainali kwenye uwanja wa Shule ya Wonder Kids, Ruangwa
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkwe Mary wakiingia kwenye uwanja wa Shule ya Wonder Kids Ruangwa kushuhudia mechi ya fainali za michuano ya kombe la Jimbo la Ruangwa kwa wanawake
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Mkewe Mary Majaliwa wakisalimiana na wachezaji wa timu ya mpira wa Miguu ya Mandawa Queens katika mechi ya fainali ya michuano ya kombe la Jimbo la Ruangwa kwenye uwanja wa Shule ya Wonder Kids Ruangwa
Judith Gideon wa Mandawa Queens (wa pili kulia) akimlamba chenga Anna Tarimo wa Mbekenyera Queens ( wa pili kushoto) katika mechi ya michuano ya Kombe la Jimbo la Ruangwa kwenye uwanja wa Shule ya Wonder Kinds Rungwa, Novemba 22, 2021. Mbekenyera Queens waliibuka na ushindi wa penati 3-1. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
…………………………………………………………
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameshuhudia Mchezo wa fainali ya Ruangwa Jimbo Cup ya Mchezo wa Mpira wa Miguu kwa upande wa wanawake kati ya Mbekenyera Queens na Mandawa Queens uliofanyika kwenye uwanja wa Shule ya msingi na awali ya Wonder kids, Ruangwa Mkoani Lindi.
Katika Mchezo huo ambao Timu ya Mbekenyera iliibuka kwa ushindi wa mikwaju ya penalti 1 kwa mitatu dhidi ya Mandawa queens baada ya dakika tisini kuisha kwa goli moja kwa moja, Mshindi wa kwanza alipewa zawadi ya Fedha taslimu shilingi milioni 2, jezi na mpira.
Mshindi wa pili alipata fedha taslimu shilingi milioni moja na nusu, jezi na mpira.
Mshindi wa tatu wa michuano hiyo ni Kitandi Queens ambaye amepata shilingi milioni moja, jezi na mpira.
Michuano hiyo ilishirikisha timu 10 kutoka katika jimbo la ruangwa.