Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akihutubia wakazi wa Wilaya ya Sikonge mkoani Tabora mara baada ya kuwasili tayari kuanza ziara ya kikazi ya siku 2 akiwa ameambatana na Wajumbe wa Sekretarieti wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa. (Picha na CCM Makao Makuu)Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akimtwisha ndoo ya maji Mwalimu Florencia Mkangwa (kushoto) kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa maji ya kisima kinachotumia umeme wa jua katika kijiji cha Simbo, Igunga mkoani Tabora ikiwa sehemu ya ziara ya kikazi ya siku 2 yenye lengo la kukagua uhai wa Chama kuanzia kwenye mashina na utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2020-2021. (Picha na CCM Makao Makuu)
Sehemu ya Viongozi na wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo (hayupo pichani) ambaye amewasili mkoani Tabora tayari kuanza ziara ya kikazi ya siku 2 akiwa ameambatana na Wajumbe wa Sekretarieti wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa. (Picha na CCM Makao Makuu)
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akizungumza na Veronica Damiani anayesoma darasa la sita katika Shule ya Msingi Mgondela iliyopo Kata ya Simbo jimbo la Manonga, Igunga mkoani Tabora. (Picha na CCM Makao Makuu)
Mbunge wa Jimbo la Manonga Ndugu Seif Khamis Gulamali (kulia) akimkabidhi Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo Kitabu kinachoelezea utekelezaji wa ilani katika jimbo la Manonga wakati wa mkutano wa shina namba 6 Tawi la Igumila, Ziba wilayani Igunga mkoa wa Tabora (Picha na CCM Makao Makuu)