Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Mhe.Dkt.Jakaya Kikwete akimtunuku degree ya Uzamivu mmojja wa wahitimu wakati wa hafla ya Mahafali ya 51 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam. Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Mhe.Dkt.Jakaya Kikwete akimtunuku degree ya Uzamivu mmojja wa wahitimu wakati wa hafla ya Mahafali ya 51 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Mhe.Dkt.Jakaya Kikwete akimtunuku degree ya Uzamivu mmojja wa wahitimu wakati wa hafla ya Mahafali ya 51 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Mhe.Dkt.Jakaya Kikwete akimtunuku degree ya Uzamivu mmojja wa wahitimu wakati wa hafla ya Mahafali ya 51 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam, Mhe.Dkt.Jakaya Kikwete akiwa katika hafla ya Mahafali ya 51 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mhe.Jaji Mstaafu Damiani Lubuva akizungumza katika hafla ya Mahafali ya 51 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo Prof.William Anangisye akizungumza wakati wa hafla ya Mahafali ya 51 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City.
Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakiwa katika hafla ya Mahafali ya 51 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
****************************
Wanafunzi wapatao 1,517 wamehitimu shahada za awali na wanafunzi wapatao 48 wamehitimu Stashahada na Astashahada katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Duru ya Nne ya Mahafali ya 51 wameshauriwa kutumia elimu ambayo wameipata kutoa ushawishi kwa jamii.
Wakati huo huo Wanafunzi wapatao 495 wamehitimu Shahada za Uzamivu, Umahiri na Stashahada za Uzamili.
Ameyasema hayo leo Makamu Mkuu wa Chuo Prof.William Anangisye wakati wa hafla ta Mahafali ya 51 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika katika ukumbi wa Mlimani City.
Amesema Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinajivunia mafanikio makubwa hasa kwa kuongeza fedha za Utafiti kutoka shilingi milioni 712.8 mwaka 2018 wakati utaratibu huu unaanza hadi kufikia zaidi shilingi bilioni tatu mwaka 2021/2022.
“Katika kuboresha na kuongeza ufanisi, mwaka huu Chuo Kikuu kimeamua kuwa kati ya fedha hizo ni kwa ajili ya uvumbuzi (Innovation) fedha ambazo zinatokana na vyanzo vya ndani vya fedha”. Amesema Prof.Anangisye
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mhe.Jaji Mstaafu Damiani Lubuva amesema Baraza limeendelea kutoa ushauri na maelekezo mbalimbali kwa Chuo ili kuhakikisha kuwa lengo la utoaji elimu, utafiti na ushauri wa kitaalamu linafanikiwa ikiwemo kuendelea kusimamia uharakishwaji wa utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Chuo ili kuboresha utoaji huduma mbalimbali, hususan utoaji wa elimu bora.
Amesema Chuo na Wanafunzi wanakabiliana na upungufu wa hosteli za wanafunzi na nyumba za kuishi wafanyakazi.
“Baraza linaendelea na juhudi mbalimbali za kuzishughulikia changamoto hizo kwa kutumia fedha inazopata Serikalini na pia kwa kutumia vyanzo vyake vya ndani”. Amesema Mhe.Lubuva.