Katibu Jumuiya ya Uhifadhi wa Mazingira Mnara Mbao Kombo Juma Maalim akisoma risala wakati walipotembelewa na Rais wa chuo kikuu cha Postdam na ujio wake katika Bustani ya Botanic iliopo Migombani Mjini Unguja .
Raisi wa Chuo kikuu cha Postdam Prof. Oliver Gunther akizungumza na jumuiya ya Uhifadhi wa Mazingira Mnara wa Mbao mara alipofika katika Bustani ya Botanic na ujio wake kutembelea.
PICHA NA FAUZIA MUSSA –MAELEZO ZANZIBAR
******************************
Rais wa Chuo Kikuu cha Postdam kutoka Ujeruman Proff. Oliver Gunther amesema mashirikiana yaliopo na Manispaa ya Mjini yatasaidia kuhifadhi na kudhibiti mazingira ya Bustani ya Botanic Migombani ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia Nchi.
Aliyasema hayo wakati wa ziara yake akiwa na ujumbe aliyofuatana nao alipotembelea katika bustani hiyo na kuangalia uhifadhi wa mazingira na kupata fursa ya kupanda miti mbalimbali ya kiasili ikiwemo miti iliopotea katika bustani hiyo.
Amesema uhifadhi wa miti husaidia kuimarisha mazingira pamoja na kuthibiti wanyama wengi wasipotee jambo ambalo huipendezesha na kuipa haiba bustani hiyo.
Nae Mstahiki Meya wa Zanzibar Ali Haji Haji amesema amefurahishwa na ugeni ulowafikia kutoka Postdam Ujerumani ambao ni marafiki wao wa muda mrefu takribani miaka 10 ,kwa kutunza na kuhifadhi mazingira ya bustani hiyo pamoja na kufanya tafiti mbalimbali za miti ya kiasili.
Aidha amesema matarajio yao kutokana na ugeni huo ni kuongeza mashirikiano ya pamoja katika kuinyanyua bustani hiyo na kuirejesha miti ya asili ambayo imekwisha toweka,
Nae Mkurugenzi wa Manispaa ya Mjini Ali Khamis Mohammed amefahamisha kuwa Chuo kikuu cha Postdam Ujerumani hutoa misaada mbali mbali ya kuimarisha bustani hiyo kwa lengo la kuirejesha hadhi yake ya awali .
Aidha alieleza Manispaa ya Mjini itaendeleza kushirikiana na wadau ili kuimarisha bustani mbali mbali zilizopo katika Manispaa hiyo,
Kwa upande wa Mkuu wa Idara ya Huduma za Jamii na Mazingira, Manispaa ya Mjini Mwanajuma Ali Abuod ameutaka Ujumbe huo kuitumia fursa hiyo kwa kufanya tafiti za kisaikolojia ya miti katika Manispaa ya Zanzibar .
“Muitumie fursa muliyoipata kwa kufanya tafiti zenu za kisaikolojia ya miti itasaidia zaidi kuitangaza Zanzibar ,’’alisema Mkuu huyo.
Alisema Ujio wa Ugeni huo utasaidia kuengeza mashirikiano kwa kubadilishana mawazo na kujifunza taaluma iliopo katika bustani ya botanic.
Nae Katibu wa Jumuiya ya Hifadhi ya Mazingira Mnara wa Mbao Kombo Juma Maalimu akieleza changamoto zilizopo ikiwemo ukosefu wa vitendea kazi , pamoja na mafunzo ya kiutaalamu ya uendeshaji wa bustani hiyo.
Vile vile alisema ukamilishwaji wa bwawa la kufugia samaki na pembea za kuchezea watoto pamoja na kukiomba Chuo Kikuu cha Postdam kuingiza Bustani ya Migombani (Botanic Garde) na ziliopo duniani ili ipatikane fursa za kimasomo na kubadilishana uzoefu .