Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo akiteta jambo na Mwenyekiti wa Shina namba 5 Ndugu Noel Tayari (kushoto) mara baada ya kuwasili kwenye kikao cha Shina hilo lililopo Tawi la Kilimani kata ya Nsemulwa,Mpanda mkoani Katavi. (Picha na CCM Makao Makuu)
Sehemu ya wakazi wa Shina namba 5, Tawi la Kilimani kata ya Nsemulwa,Mpanda mkoani Katavi ambao wamehidhuria mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Daniel Chongolo. (Picha na CCM Makao Makuu)
***********************
Katibu mkuu wa chama cha mapinduzi daniel chongolo amekubaliana na ombi la viongozi wa mkoa wa katavi kuuwezesha mkoa huo kuwa na vihenge na maghala ya kanda kwa ajili ya kihifadhi mazao yao mahindi.
Chongolo amepokea maombi hayo baada ya mkuu wa mkoa wa katavi kutoa ombi hilo kwa chama cha mapinduzi ili kuhimiza wizara kuidhinisha kwa haraka maombi hayo kwani, kwa kufanya hivo itasaidia wakulima kupata huduma hiyo kwa ukubwa ambapo wakala wa wakala wa taifa wa hifadhi ya chakula (NFRA) itakuwa karibu zaidi tofauti na ilivyo sasa ukilinganisha na uzalishaji mkubwa wa mahindi katika mkoa wa katavi, mikoa jirani na namna mkoa huo unavyofunguka kwa kasi.
Aidha chongolo ameitaka NFRA, kuanza kutafsiri kwa vitendo namna miradi hii ya ujenzi wa maghala inavyoleta matokeo chanya, kwa sababu haitakuwa busara kuwepo na vihenge kama hivi alafu mwaka kesho wananchi waanze kulalamika pa kuuza mahindi au mazao yao, ni lazima kuweka mpango mapema wa kununua na kuhifadhi mahindi na sio kusubiri mpaka muda unapofika mwisho ndio mnaanza kukimbizana.
Mkuu wa mkoa wa katavi mwanamvua mrindoko akizungumza kuhusu mradi huo, ameeleza kwa mpaka kufikia mwezi machi mwakani vihenge hivyo vitakuwa tayari vimeanza kufanya kazi, lakini pia amemuomba Chongolo kuwasaidia kusukuma maombi hayo ya kuifanya katavi kuwa kanda ya ununuzi wa mazao kupitia NFRA.
Mradi huo wa vihenge sita vyenye uwezo wa kuhifadhi tani 3300 kila kimoja, sawa na tani elfu 20000 ulianza kujengwa 14 januari 2019 amnapo unatarajiwa kukamilika tarehe 31 machi 2022, na unagharimu shilingi bilioni 14, ambapo mpaka sasa mradi umetekelezwa kwa asilimia 95 kwa vihenge na asilimia 80 miundombinu mingine.
Aidha Katika hatua nyingine chongolo amesisitiza matumizi mazuri ya fedha za ndani za halmashauri ambapo amesema ni lazima zisimamiwe ipasavyo ili zilete matokeo chanya ya ujenzi wa miradi ya maendeleo kama ilivyotarajiwa, ambapo amefurahishwa na ujenzi wa kituo cha afya cha Nsemurwa ambacho kinajengwa kwa kutumia mapato ya ndani huku ujenzi ukienda kwa kasi na kwa ubora.
Chongolo ameeleza hayo, baada ya kutembelea na kukagua ujenzi wa kituo hicho kinachojengwa kwa kutumia mapato ya ndani kwa gharama ya shilingi milioni 400 kichoanza septemba 8, 2021 na kinatarajiwa kukamilika februari mwakani.