Meneja Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS) ,Ally Kebby akimkabidhi vifaa mbalimbali vya TEHAMA vyenye thamani ya shilingi Milioni 37.7 Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya sayansi ya Afya Mvumi Prof.Charles Mazengo vilivyotolewa Mradi wa HPSS leo November 18,2021.
Meneja Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS) ,Ally Kebby akishuhudia Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya sayansi ya Afya Mvumi Prof.Charles Mazengo akiwakabidhi wanafunzi wa taasisi hiyo vifaa vya TEHAMA vyenye thamani ya shilingi Milioni 37.7 vilivyotolewa Mradi wa HPSS leo November 18,2021.
Meneja Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS) ,Ally Kebby akimuonyesha vifaa mbalimbali vya TEHAMA Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya sayansi ya Afya Mvumi Prof.Charles Mazengo vilivyotolewa leo November 18,2021 na Mradi wa HPSS katika taasisi hiyo.
Meneja Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS) ,Ally Kebby akizungumza mara baada ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya TEHAMA vyenye thamani ya shilingi Milioni 37.7 katika Taasisi ya Mafunzo ya sayansi ya Afya Mvumi leo November 18,2021.
Meneja Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS) ,Ally Kebby akielezea vifaa hivyo jinsi vitakavyoijengea uwezo Taasisi hiyo kutoa mafunzo kwa kizazi kipya cha wataalam katika fani ya uhandisi wa vifaa Tiba leo November 18,2021.
Meneja Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS) ,Ally Kebby akimsikiliza Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya sayansi ya Afya Mvumi Prof.Charles Mazengo mara baada ya kupokea vifaa vya TEHAMA vyenye thamani ya shilingi Milioni 37.7 vilivyotolewa Mradi wa HPSS leo November 18,2021.
Mwanafunzi wa kozi ya Uhandisi wa Vifaa Tiba,Fahad Urassa akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wanafunzi wenzake mara baada ya kupokea vifaa vya TEHAMA vyenye thamani ya shilingi Milioni 37.7 vilivyotolewa Mradi wa HPSS leo November 18,2021.
Meneja Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS) ,Ally Kebby akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhi vifaa mbalimbali vya TEHAMA vyenye thamani ya shilingi Milioni 37.7 katika Taasisi ya Mafunzo ya sayansi ya Afya Mvumi leo November 18,2021.
………………………………………………………
Na.Alex Sonna,Mvumi
Mradi wa Tuimarishe Afya (HPSS) imekabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vya TEHAMA vyenye thamani ya shilingi Milioni 37.7 kwa Taasisi ya Mafunzo ya Sayansi ya Afya Mvumi Dodoma.
Mradi huo ni mradi wa ushirikiano kati ya Tanzania na Uswiss unaofadhiliwa na Serikali ya uswisi kupitia shirika lake la maendeleo na ushirikiano(SDC) na kutekelezwa na Taasisi ya Tropical and Public Health (Swiss TPH).
Akikabidhi Vifaa hivyo leo November 18,2021 Meneja mradi wa HPSS,Ally Kebby amesema kuwa vifaa hivyo vitaijengea uwezo Taasisi hiyo kutoa mafunzo kwa kizazi kipya cha wataalam katika fani ya uhandisi wa vifaa Tiba ambayo ni muhimu katika utoaji wa huduma za afya na matibabu nchini.
“Msaada huu utaiwezesha Taasisi ya mafunzo ya Sayansi ya afya Mvumi kuimarisha uwezo wake na kuendeleza mafunzo ya umahiri kwa lengo la Kuwajengea wanafunzi ujuzi unaohitajika katika fani ya uhandisi wa vifaa tiba nchini Tanzania,”amesema Kebby.
Bw.Kebby amevitaja vifaa hivyo vilivyokabidhiwa ni pamoja na kompyuta mpakato,projekta na skrini ya projekta,ambavyo vitasaidia kwa kiasi kikubwa katika kuboresha mafunzo ya kozi ya uhandisi wa vifaa tiba iliyoanzishwa hivi karibuni katika Taasisi hiyo kwa nia ya kukabiliana na uhaba wa rasilimali watu katika sekta ya afya na matibabu nchini.
“Mradi wa HPSS unatekelezwa nchini tangu mwaka 2011 kwa kushirikiana na Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,wazee na Watoto pamoja na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa katika kuimarisha mfumo ya afya nchini kwa kuwekeza katika uboresha wa usimamizi na Menejimenti ya sekta ya afya na kujengea uwezo wataalam wanahuduma katika sekta ya afya,”ameeleza
Aidha Amefafanua kuwa awali mradi wa HPSS umeisaidia Taasisi ya mafunzo ya Sayansi ya Afya Mvumi katika kuandaa mtaala wa kozi ya uhandisi wa vifaa tiba ,uboreshaji wa miundombinu ya mafunzo, utoaji wa vifaa vya karakana na vitendea kazi kwajili ya mafunzo kwa vitendo pamoja na vitabu vya kufundishia na rejea.
“Na hadi sasa mradi umechangia ufadhili wa masomo kwa kundi la kwanza la wanafunzi wa kozi ya uhandisi wa vifaa tiba na tayari Taasisi ya Sayansi ya afya ya mvumi imesajili wanafunzi 11 kwajili ya program ya mafunzo ya uhandisi wa vifaa tiba,”.
Kwa upande wake Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya sayansi ya Afya Mvumi Prof.Charles Mazengo ,amesema kuwa vifaa hivyo ni msaada mkubwa kwao katika ufundishaji kwani hadi sasa tayari ina wanafunzi 7 mwaka wa kwanza na wako 6 mwaka wa pili.
“HPSS wameanza na sisi hivyo hatutabaki tu kusubilia msaada bali na sisi tutajiongeza kutafuta na vifaa vingine,”ameeleza.
Naye Mwalimu wa kozi ya Uhandisi Vifaa Tiba Salum Pwacha amesema Taasisi hiyo pekee ndio inatoa kozi hiyo hivyo itasaidia kufika mbali kwa Taifa letu kwasababu katika hospitali nyingi vifaa tiba huwa vinaharibika.
”Vifaa tiba vikiharibika hakuna wataalamu wa kutengeneza lakini kupitia kozi hiyo itasaidia kutoa wataalamu watakaoweza kusaidia kutengeneza vifaa tiba katika hospitali mbalimbali nchini vinapoharibika”amesema
Mwanafunzi wa kozi hiyo,Fahad Urassa ametoa shukrani kwa HPSS kwa kutoa msaada huo ambao utawasaidia katika kujifunza kwa vitendo zaidi na aliahidi kutoa ushirikiano katika kozi hiyo ya vifaa tiba.