WAZIRI wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo,akizungumza na waandishi wa habari leo November 17,2021 jijini Dodoma kuhusu mafanikio ya Sekta ya Viwanda na Biashara katika kipindi cha miaka 60, ya uhuru wa Tanganyika.
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo,(hayupo pichani) wakati akiwasilisha mafanikio ya Sekta ya Viwanda na Biashara katika kipindi cha miaka 60, ya uhuru wa Tanganyika leo November 17,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Prof. Kitila Mkumbo ,akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo November 17,2021 jijini Dodoma wakati akizungumzia mafanikio ya Viwanda na Biashara katika kipindi cha miaka 60, ya uhuru wa Tanganyika.
…………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
WIZARA ya Viwanda na Biashara imesema katika kipindi cha miaka 60 ya uhuru wa Tanzania Bara imepata mafanikio ndani ya miaka 60 msukumo mkubwa wa ujenzi wa uchumi wa viwanda, idadi ya ajira imeongezeka zaidi na kufikia ajira 482,601 mwaka 2021.
Hayo yameelezwa leo Jumatano ,Novemba 17,2021 jijini Dodoma na na Waziri wa Viwanda na Biashara,Prof. Kitila Mkumbo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu mafanikio ya Sekta ya Viwanda na Biashara katika kipindi cha miaka 60, ya uhuru wa Tanganyika.
AJIRA NA VIWANDA
Waziri Kitila amesema ajira katika Sekta ya Viwanda imeendelea kuongezeka ambapo mwaka 1961 Sekta ya Viwanda ilichangia asilimia 9 ya ajira zote nchini. Hadi kufikia mwaka 2015, ajira katika Sekta ya Viwanda zilikuwa zimeongezeka na kufikia ajira 254,786.
Aidha, kutokana na msukumo mkubwa wa ujenzi wa uchumi wa viwanda, idadi ya ajira imeongezeka zaidi na kufikia ajira 482,601 mwaka 2021.
“Viwanda vyetu vingi vinamilikiwa na watanzania lakini katika sekta biashara sio muhimu nani anamiliki muhimu kwetu ni uwekezaji upo hapa Tanzania bila kujali anatoka nchi gani,muhimu sisi awe ameajiri watanzania,”amesema
Waziri Kitila amesema watanzania wengi wamepata ajira za moja kwa moja rasmi na zisizo rasmi kupitia sekta ya viwanda.
“Tumefanya hesabu katika viwanda vyetu walioajiriwa ni asilimia 99,ukija kwenye viwanda vikubwa pia wengi ni watanzania na muhimu sio nani anamiliki,kikubwa analipa kodi hela inazunguka ndani ya Tanzania.
“Kwa ujumla watu ambao wameajiriwa katika viwanda ni 400,000 lakini uzuri wa viwanda vinazalisha ajira za moja kwa moja zisizorasmi,”amesema
VIWANDA NA PATO LA TAIFA
Waziri huyo amesema mchango wa Sekta ya Viwanda kwenye Pato la Taifa umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka ambapo wakati wa Uhuru mwaka 1961, Sekta ya Viwanda ilikuwa ikichangia asilimia 3.5 ya Pato la Taifa (GDP). Amesema hadi kufikia mwaka 2015 mchango wa sekta hiyo ulikuwa asilimia 7.9.
Amesema kutokana na jitihada za Serikali za kuhamasisha ujenzi wa viwanda mchango wa sekta ya viwanda kwenye Pato la Taifa uliongezeka na kufikia asilimia 8.5 ya Pato la Taifa mwaka 2019. Mwaka 2020 mchango wa sekta ulishuka kidogo hadi asilimia 8.4.
SERIKALI HAIFANYI BIASHARA
Aidha,Waziri Kitila amesema Serikali haifanyi biashara na wala haiwezi kuibana sekta binafsi katika utendaji kazi wake bali kumekuwa na tofauti ya tafsiri.