Mkuu wa wilaya ya Morogoro Mheshimiwa Albert Msando kushoto akimpongeza mkazi wa Mikumi mkoani humo Luka Andrea Lutuli katikati kwa kushinda sh Milioni 10 kutoka kwenye bahati nasibu ya Biko. Makabidhiano hayo yalifanyika mkoani Morogoro katika tawi la NBC. Mwingine kushoto ni Kajala Masanja balozi wa mchezo huo wa Biko.
Mkazi wa Mikumi mkoani Morogoro Luka Andrea Lutuli mwenye kofia na fulana ya biko akionyesha furaha yake baada ya kupokea fedha zake jumla ya sh milioni 10 alizoshinda kutoka kwenye bahati nasibu hiyo ya aina yake. Kushoto kwa mshindi ni Kajala Masanja Balozi wa Biko na kushuhudiwa na marafiki pamoja na majirani dukani kwa mshindi huyo. Picha na Mpigapicha wetu.
*********************************
Mkuu wa wilaya Morogoro aishauri Biko kurudisha kwa jamii
Mwandishi Wetu, Morogoro
Wakati Mkuu wa wilaya Morogoro Mheshimiwa Albert Msando akiipongeza Biko kwa kuendesha bahati nasibu ya wazi inayotoa ushindi wa urahisi kulinganisha na michezo mingine ya kubahatisha, aliwataka waendeshaji wa mchezo huo wa kubahatisha warudishe faida kidogo kwa jamii ili kuhakikisha kuwa nchi inasonga mbele kwa kutumia fursa hiyo ya michezo ya kubahatisha.
Mheshimiwa Msando aliyasema hayo ofisini kwake wakati anazungumza na mshindi wa sh milioni 10, Luka Andrea Lutuli alizoshinda kwenye droo kubwa ya Jumapili iliyopita, ambapo makabidhiano ya fedha hizo yalifanyika katika bank ya NBC, Tawi la Morogoro Mjini.
“Tunajua biko mnafanya mchezo mzuri unaotoa fedha kwa Watanzania wote, wakiwapo kutoka mkoani kwetu Morogoro na tukiri hatujawahi kusikia biko inalalamikiwa kuhusu kutotoa zawadi zenu, ila ni vyema pia mkarudisha faida kwa jamii ili nchi ijivunie zaidi uwapo wenu,” Alisema.
Biko ni mchezo wa kubahatisha unaoongoza kutoa fedha nyingi kwa Watanzania, ambapo zwadi za papo kwa hapo zinatoka kila sekunde moja kuanzia sh 2500 hadi milioni 5 papo hapo bila kusahau kutoa zawadi ya hadi sh milioni 40 kila Jumapili ambapo mbali na kucheza kwa namba ya Kampuni 505050 na kumbukumbu 2456, pia watu wanaweza kucheza live kwa kuingia www.biko.co.tz.
Bahati nasibu ya biko inachezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kuanzia sh 1000 na kuendelea, ambapo baada ya kuchungulia nafasi kwa www.biko.co.tz, mchezaji ataweka namba ya simu na fedha kuanzia sh 1000 na kuendelea na kubonyeza kitufe cha Cheza Sasa ili awahi nafasi za ushindi.