Fredy Mgunda,Iringa.
CHAMA
cha Waalimu CWT Wilaya ya Kilolo Kimeabainisha kuwepo kwa changamoto ya
Miundombinu katika Sekta ya Elimu ikiwemo ukosefu wa vyumba vya kutosha vya
madarasa hali inayowalazimu baadhi ya wanafunzi kusomea chini ya mti jambo
ambalo linarudisha nyuma maendeleo ya elimu katika wilaya hiyo
Akizungumza
wakati mafunzo kwa walimu wawakilishi mahali pa kazi yanayoendeshwa na chama
cha Walimu Wilaya ya kilolo (CWT), Katibu wa Chama CWT Anton Mangw`alu alisema
kuwa wilaya ya hiyo ina na changamoto lukuki kama vile uhaba wa vyumba wa
kusomea wanafunzi,shule kuwa na kitabu kimoja cha hisabati jambo
linalozorotesha ufanisi kwa walimu.
Alisema
kuwa baadhi ya shule kama shule ya msingi Kidabaga na shule ya msingi ya Lyamko
iliyopo kata ya Bomalang’ombe zinakabiliwa na uhaba wa vitabu vya kufundishia
masomo wanafunzi ambao shule zote hizo zinakitabu kimoja kimoja cha hisabati
kwa kila darasa jambo linalozorotesha ufanisi kwa walimu.
Mwalimu
Mangw`alu alisema kukosekana kwa vitabu vya kutosha katika shule nyingi zilizopo
wilaya ya kilolo kunachangia kwa kiasi kikubwa wanafunzi wengi kushindwa
kufaulu mitihani ya taifa kutokana na wanafunzi wengi kushindwa kuwafundisha
vizuri na walimu kwa ajili ya ukosefu wa vitabu husika.
Alisema
kuwa changamoto nyingine ni kukosekana kwa vyumba vya madarasa jambo ambalo
linachangia wanafunzi wengine kuso mea chini ya miti jambo ambalo sio sawa
kabisa kwa wakati uliopo kwa mfano shule ya msingi Lukoga haina vyumba vya
madarasa kabisa na wanafunzi wake
wanasomea chini ya miti na shule ya msingi Kitelewasi hakuna kabisa vyoo vya
walimu jambo ambalo linawaweka katika mazingira magumu walimu wakati wa
kufundisha.
“Kwa
mazingira kama hayo ndugu zangu waandishi wa habari lazima walimu watakuwa na
wakati mgumu wakati wa kufundisha wanafunzi hawana vyoo,hakuna vyumba vya
madarasa,maslai yao bado duni,hivyo ni lazima serikali ya wilaya ya kilolo
kuhakikisha inatafuta namna ya kutatua changamoto hizo” alisema mwalimu Mangw`alu
Mwalimu
Mangw`alu alisema licha ya changamoto hizo bado walimu wa wilaya ya Kilolo
wamekuwa wakitumia jitihada binafsi na kuhakikisha wanafunzi wanafanya vizuri
kwenye mitihani yao na kufanya vizuri kitaifa.
Aidha
Mwalimu Mangw`alu aliiomba serikali ya wilaya ya kilolo kuboresha mazingira ya walimu
wawapo kazini na kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo pamoja na zile zinazohusu
maslahi ya waalimu ili kusaidia ukuaji wa taaluma na ubora
Licha
ya changamoto hizo chama cha walimu wilaya ya Kilolo (CWT) wamempongeza Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kuwapandisha
madaraja na kuongeza ajira za walimu kwa kipindi kifupi ambacho yupo
madarakani.
Kwa
upande wake mwenyekiti wa chama cha walimu wilaya ya Kilolo (CWT) Mtemi Mgalula
alisema kuwa wanafunzi wa baadhi ya shule wamekuwa wanakumbana na changamoto ya
kufanya mitihani kwenye vyumba vya madarasa ambavyo havina madirisha wala
milango hivyo ukitokea upepo wanafunzi wanakuwa kwenye mazingira magumu.
“Ukipiga
upepo karatasi zile ni kukimbiza nazo kwa kuwa darasa hayana madirisha,fremu Wala
milango kwa kuwa hakuna kitu ambacho kinauwezo wa kuzuia upepo katika madarasa
hayo” alisema Mgalula
Alisema
kuwa wamekuwa wakipokea malalamiko mara kwa mara juu ya changamoto ya
miundombinu ambavyo imekuwa ikiwaweka walimu katika mazingira magumu ya
ufundishaji kwa wanafunzi husika.
Mwalimu
Mgalula alisema kuwa bado walimu wa wilaya hiyo wanadai madai ya uhamisho
ambayo hadi sasa hawajalimu mfano ya walimu waliohamishwa kutoka shule ya
sekondari kwenye shule ya msingi jumla walimu 99 walihamishwa na walimu 26 tu ndio
waliolipwa stahiki zao lakini wote waliobaki bado hawajalipwa madai yao.
Aidha
Mwalimu Mgalula alisema kuwa zoezi la sensa ni muhimu sana kwa taifa kujua
idadi ya wakazi kwa ajili ya kupanga mipango ya kuleta maendeleo kwa wananchi
hivyo jukumu la walimu kumuunga mgono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kufanikisha zoezi hilo kwa asilimia 100.
Alisema
kuwa walimu wanapaswa kuendelea kutoa elimu ya madhara ya ukatili wa kijinsia
kwenye jamii ambazo wanaishi nazo huku ili kuwa na kizazi ambacho kitakuwa na
maadili bora nakutomeza kabisa maswala yote ya ukatili wa kijinsia.
Mwalimu
Mgalula alisema walimu wanatakiwa kuendelea kuwa na maadili bora ili kuwasaidia
wananchi wengine kuiga mfano wao kwa namna ya kufanya kazi kwa kujituma na
kulijenga taifa kiuchumi na kielimu.
Alisema
kuwa rushwa ni adui wa maendeleo ya wananchi wote hivyo walimu wanatakiwa kuwa
matari wa mbele kuhakikisha wanapinga vitendo vyote vyenye viashiria vya
rushwa.
Naye
mgeni rasmi mkuu wa wilaya ya kilolo ambaye aliwakilishwa na afisa tarafa ya
Mazombe Silvanus Kingu’ung’e aliwataka walimu kuwa mabalozi wa kukemea vitendo
viovu vinavyofanywa na baadhi yao ikiwemo kujihusisha kingono na wanafunzi
kwani tabia hiyo inadharirisha taaluma yao.
Kingu’ung’e
alisema kuwa waalimu wenye maadili ni lazima wajikite kwenye uzalendo na
uadilifu ili kuwa mfano bora kwa jamii
Alisisitiza
kuwa viongozi wa CWT wanatakiwa kuweka mikakati ya kuwabaini waalimu
wanaojihusisha kimapenzi na wanafunzi ili kukomesha tabia hiyo ya unyanyasaji
na ukatili unaokatisha ndoto za wanafunzi hasa wa kike
Kingu’ung’e
alisema kuwa ni aibu kusikia mwalim ana mahusiano ya ki ngono na mwanafunzi
jambo hilo limekuwa likiitia doa kada ya ualimu kwa vitendo amvyo vinafanywa na baadhi ya walimu kwa wanafunzi.
alisisitiza
kuwa waalimu wote wanatakiwa kuwa mfano bora wa kuigwa na jamii kwa kukemea vitendo vya ukatili na mmomonyoko wa
maadili katika jamii.
Kingu’ung’e
alimtaka mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kilolo kuhakikisha anazitatua
mara moja changamoto za walimu kwa kuwa walimu wanamchango mkubwa kwenye
maendeleo ya taifa la Tanzania.
Alikiri
uwepo wa uhaba wa vitendea kazi na kuahidi kulifanya kazi jambo hilo na
kulitatua mara moja tatizo hilo kwa ajili ya maendeleo ya elimu kwa wanafunzu
wa wilaya ya Kilolo.
Kingu’ung’e
aliwataka walimu kuendelea kufundisha kwa moyo wote huku serikali ikiendelea
kutatua changamoto ambazo zimekuwa zinawakumba walimu wa wilaya ya Kilolo
kuanzia miundombinu,mazingira ya shule na kuboresha maslai ya walimu kwa ajili
ya kuboresha sekta ya elimu katika wilaya hiyo.