******************************
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi amepokea Vikombe vitatu ambavyo amekabidhiwa na Viongozi wa timu ya Wizara pamoja na wachezaji walioshiriki Mashindano ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) mwaka 2021 yaliyofanyika Manispaa ya Morogoro.
Dkt. Abbasi amepokea vikombe hivyo leo Novemba 16, 2021 katika ofisi za Wizara hiyo Mtumba Jijini Dodoma ambavyo ni Kombe la mshindi wa tatu kwa Mchezo wa Netiboli na vikombe viwili vya mchezo wa Karata kwa wanawake, na kuwahimiza wanamichezo kuendelea na moyo wa kufanya mazoezi ili kuwa na timu bora zaidi.
Tukio hilo pia limehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Ally Possi.