Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Dodoma anaeshughulikia uchumi,Aziza Mumba,akifungua mafunzo ya wajasiriamali wazalishaji na wasindikizaji wa Zabibu na bidhaa za zabibu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Antony Mtaka yaliyoanza leo Novemba 15,2021 Jijini Dodoma.
Meneja wa Shirika la Viwango (TBS) Kanda ya Kati Bw.Nickonia Mwambene,akitoa taarifa kuhusu mafunzo ya wajasiriamali wazalishaji na wasindikizaji wa Zabibu na bidhaa za zabibu yaliyoanza leo Novemba 15,2021 Jijini Dodoma.
Baadhi ya waashiriki wakifatilia mada mbalimbali wakati wa mafunzo ya wajasiriamali wazalishaji na wasindikizaji wa Zabibu na bidhaa za zabibu yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango (TBS) yaliyoanza leo Novemba 15,2021 Jijini Dodoma.
Meneja wa Shirika la Viwango (TBS) Kanda ya Kati Bw. Nickonia Mwambene,akitoa elimu kuhusu Soko la pamoja na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC Common Market) wakati wa mafunzo ya wajasiriamali wazalishaji na wasindikizaji wa Zabibu na bidhaa za zabibu yaliyoanza leo Novemba 15,2021 Jijini Dodoma.
Afisa Viwango TBS Bi.Lilian Gabriel,akitoa mada wakati wa mafunzo ya wajasiriamali wazalishaji na wasindikizaji wa Zabibu na bidhaa za zabibu yaliyoanza leo Novemba 15,2021 Jijini Dodoma.
Afisa Biashara kutoka jiji la Dodoma Amir Kibwana,akitoa mada kuhusu usajili wa Biashara wakati wa mafunzo ya wajasiriamali wazalishaji na wasindikizaji wa Zabibu na bidhaa za zabibu yaliyoanza leo Novemba 15,2021 Jijini Dodoma.
Meneja wa Shirika la Viwango (TBS) Kanda ya Kati Bw.Nickonia Mwambene,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa mafunzo ya wajasiriamali wazalishaji na wasindikizaji wa Zabibu na bidhaa za zabibu yaliyoanza leo Novemba 15,2021 Jijini Dodoma.
Mkurugenzi Ugogoni Wine Lissa Peter,akielezea jinsi walivyopata elimu wakati wa mafunzo ya wajasiriamali wazalishaji na wasindikizaji wa Zabibu na bidhaa za zabibu yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango (TBS) yaliyoanza leo Novemba 15,2021 Jijini Dodoma.
Mshiriki wa Mafunzo kutoka Jimbo Katoliki Novatus John,akizungumza mara baada ya kupata mafunzo ya wajasiriamali wazalishaji na wasindikizaji wa Zabibu na bidhaa za zabibu yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango (TBS) yaliyoanza leo Novemba 15,2021 Jijini Dodoma.
Afisa Kilimo jiji la Dodoma Bi.Agnes Woisso,akielezea kanuni za kilimo bora wa mafunzo ya wajasiriamali wazalishaji na wasindikizaji wa Zabibu na bidhaa za zabibu yaliyoandaliwa na Shirika la Viwango (TBS) yaliyoanza leo Novemba 15,2021 Jijini Dodoma.
Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Dodoma anaeshughulikia uchumi,Aziza Mumba,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua mafunzo ya wajasiriamali wazalishaji na wasindikizaji wa Zabibu na bidhaa za zabibu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Antony Mtaka yaliyoanza leo Novemba 15,2021 Jijini Dodoma.
………………………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) limetoa mafunzo kwa wajasiriamali wazalishaji na Wasindikizaji wa Zao la Zabibu Mkoani Dodoma lengo likiwa ni kujua namna bora ya kuzalisha zabibu na bidhaa zinazotengenezwa na zao.
Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo leo Novemba 15,2021 Jijini Dodoma kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Antony Mtaka, Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Dodoma anaeshughulikia uchumi,Aziza Mumba ,amesema azma ya Serikali ni kuhakikisha inaongeza thamani kwenye zao la zabibu.
Bi.Mumba amesema uongozi wa Mkoa unaamini mafunzo hayo ni njia muafaka ya kuleta tija pamoja na kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuhakikisha kuwa zao la zabibu na bidhaa zake zinakuwa na mchango katika pato la mtu mmoja mmoja pamoja na taifa kwa ujumla.
“Kwa hiyo nitoe rai kwenu nyie washiriki wa mafunzo haya kwamba Nchi yetu kufikia uchumi wa kati iwe chachu ya kutufanya tuendelee kufanya kazi kwa bidii na maarifa ili uchumi wa Nchi na mtu binafsi uendelee kukaa na kufikia ngazi moja nan chi zenye uchumi wenye nguvu duniani,”amesema Bi.Mumba
Kwa upande wake Meneja wa Shirika la Viwango (TBS) Kanda ya Kati Mkoa wa Dodoma Bw. Nickonia Mwambene amesema lengo la mafunzo hayo ni kuwapa elimu wajasiriamali namna ya kuzalisha zabibu na bidhaa zinazotengenezwa na zao hilo zenye ubora.
“Lengo kubwa ni wajasiriamali wapate elimu ya uzalishaji ndio maana tuna wataalamu wa kilimo,afya,usalama na watu wa Tamisemi ili tuweze kutoa elimu kwa pamoja juu ya viwango vya ubora na wanaweza kuuza ndani na nje ya Nchi.
Amesema mafunzo hayo yatawasaidia wajasiriamali kupata soko kubwa na kujua mnyororo wa thamani wa zao hilo ikiwa ni pamoja na kulima kilimo bora na zabibu bora zenye ubora.
“”Tumewaambia soko la Dodoma sio la kwetu tu ni la Afrika Mashariki hivyo ni lazima wakachakate bidhaa ambayo itashindana na bidhaa za nje,”amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Ugogoni Bi. Lissa Peter ameishukuru TBS kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo yatawasaidia kupata elimu namna bora ya kuzalisha bidhaa zinazotokana na zao la zabibu.
“Ningependa kuwakaribisha wadau katika bishara hii kwani inafaida kubwa na itapelekea kuongeza pato la Taifa ningependa kuwakaribisha wadau katika biashara hii,”amesema
Naye Afisa Kilimo wa Jiji la Dodoma,Agness Woisso amesema wataalamu wanasema mvinyo mzuri unaanzia shambani hivyo ni lazima wakulima waweze kujua ni namna gani watazalisha zabibu nzuri .
Amesema kuwa huko nyuma walikuwa na changamoto ya kutokujua zabibu bora lakini kwa sasa wanaenda kuwafundisha jinsia bora za kuzalisha zabibu.
“Manufaa kwa hapa kwetu mkulima wa kawaida mwenye ekari moja anaweza kupata tani nne mpaka sita tutaendelea kutoa elimu nawashukuru TBS kwani mafunzo haya yanawasaidia kujua ni muda gani wa kupuliza dawa,”amesema
Naye, Novatus Karebo kutoka Jimbo Kuu Katoliki Kondoa,amesema mafunzo hayo yatawasaidia kujua soka la ndani na nje linataka nini.
“Nitoe Wito kwa wazalishaji wenzangu tuhakikishe tunakidhi vigezo vyote vinavyotakiwa na namna bora ya kuchakata mvinyo kwa kiwango cha kimataifa na namna bora ya kufuata katika zao hilo,”amesema.