**************************
Happy Lazaro,Arusha.
Arusha.Mwanafunzi wa kidato Cha tatu shule ya Sekondari ya Suye katika Jiji la Arusha,Evance Florian(17) ameuawa kwa kipigo alipokuwa anadaiwa sh 3000.
Kamanda wa Polisi mkoa Arusha, Justin Masejo akizungumza na mwananchi Leo 14 Novemba amesema mwanafunzi huyo amefariki Jana Novemba 13, 2021akiwa anapatiwa matibabu hospitali ya rufaa ya Mountmeru kutokana na kipigo.
Amesema Jeshi la Polisi Mkoa Arusha linamshikilia mwanafunzi wa chuo Cha ufundi Arusha, Ibrahim Shaban (18) kwa kuhusika kumpiga Florian Aliyekuwa anamdai.
Kamanda Masejo amesema uchunguzi wa tukio hilo ukikamilika jarada la mtuhumiwa huyo litafikishwa katika ofisi ya mashitaka Kwa hatua zaidi za kisheria.
Amesema mwili wa kijana aliyeuawa umehifadhiwa Katika hospitali ya rufaa ya Mountmeru Kwa taratibu za mazishi.
“Tunaonya watu waache kujichukukia sheria mkononi hatua za kisheria zitaendelea kuchukuliwa kwa wahusika”amesema.