***************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Wanamichezo mbalimbali wakiongozwa na viongozi wa klabu ya Simba wamejitokeza kwa wingi katika mazishi ya mama yake mzazi wa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba Sc Barbara Gonzalez aitwaye Rhoda Yahya Lambert yaliyofanyika katika makaburi ya Kisutu Jijjini Dar es Salaam.
Miongoni mwa viongozi ambao wameshiriki katika mazishi hayo ni pamoja na kocha mpya wa klabu hiyo Pablo Franco akiongozana na kocha msaidizi Thierry Hitimana pamoja na viongozi wengine.
Msiba ulitokea leo asubuhi nyumbani kwake Kigamboni JJijini Dar es Salaam