***********************
Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta ya Binafsi (TPSF) wameandaa TUZO za ubora wa viwango kwa nchi wanachama wa nchi za kusini mwa Afrika (SADC) tuzo zenye lengo la kutambua na kukuza sekta ya biashara kupitia ubora wa aidha na huduma katika ukanda huo kwa mwaka 2020/2021.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es Salaam Meneja Udhibiti Ubora TBS, Bw.Gervas Kaisi amesema tuzo hizo ni sehemu ya mipango ya serikali katika kuboresha huduma na bidhaa zinazozalishwa hapa nchini kupitia matumizi ya viwango pamoja na kanuni za ubora kwa taasisi za umma za sekta binafsi ili kuhakikisha kuwa mifumo bidhaa na huduma zinakidhi mahitaji ya kitaifa,kikanda na Kimataifa hali itakayopelekea kufanya vizuri kwenye masoko ya ngazi zote.
“Moja ya tuzo zitakazotolewa ni pamoja na tuzo za kampuni bora ya mwaka,tuzo kwa bidhaa bora za mwaka, tuzo kwa huduma bora za mwaka, tuzo kwa bidhaa bora za mwaka, tuzo kwa huduma bora za mwaka,muuzaji bora wa mwaka nje ya nchi pamoja na tuzo ya mtu mmoja aliyefanya vizuri katika sekta ya ubora kwa hapa nchini”. Amesema
Aidha amesema Mashindano yatazinduliwa rasmi Novemba 15,2021 na mgeni rasmi katika uzinduzi huo anatarajiwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo katika Ofisi za TBS makao Makuu Jijini Dar es Salaam.