Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila akipokea Mwenge wa Uhuru kutoka kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Ally Hapi , mpakani mwa Mkoa wa Mara na Simiyu.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. David Kafulila akimkabidhi Mwenge wa uhuru, Mkuu wa Wilaya ya Busega Mhe. Gabriel Zakaria, wilaya ambayo ipo
mpakani na Mkoa wa Mara, June 28,2021.
*******************************
Mkuu wa Mkoa Simiyu, Mhe.David Kafulila, leo amewapongeza wakurugenzi wa wakuu wa wilaya 5 za Mkoa wa Simiyu kwa kuendelea kuboresha usimamizi wa utekelezaji wa miradi ya maendeleo na kusisitiza kuwa ni juhudi hizo zilizofanikisha mkoa wa simiyu kushika nafasi ya 4 mwaka huu 2021 kutoka nafasi ya 20 mwaka 2019.
” Mimi naona fahari kuwa na timu hii ya wakuu wa wilaya na wakurugenzi. Mbali ya kupaisha mkoa huu kutoka nafasi ya 2 kutoka mwisho mwaka 2020 mpaka nafasi ya 2 juu katika makusanyo ya halmashauri kimkoa, leo nimepata taarifa kuwa mkoa wetu umeshika nafasi ya 4 kitaifa katika miradi ya mwenge iliyokaguliwa kulinganisha na nafasi ya 20 mwaka 2019.
Naamini mwakani tutashika nafasi ya 1.” Angalia hapa Busega, taarifa ya makusanyo ya robo ya mwaka wa fedha 2020 ilikuwa asilimia 15% ya lengo, kulinganisha na asilimia 29% kwenye robo ya kwanza mwaka 2021.
Hivyo inawezekana. Tuendelee kupambana kujenga mkoa wetu ” alisisitiza Kafulila.Mwisho.