****************************
Ni katika ukaguzi wa baadhi ya miradi ya maendeleo ikiwa Leo mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Bukoba vijijini ambae pia ni Mwenyekiti wa ARAT TAIFA Mh.Murshid Ngeze amesema Toka awe mwenyekiti wa halmashauri hiyo hajawai kuona fedha nyingi namna hiyo kutoka katika mapato ya ndani ya halmashauri kwa ajili ya maendeleo.
Akizungumza na Wananchi wa Kijiji hicho Cha Mulahya kata Katerero mkoani Kagera Mh.Murshid Ngeze amesema wananchi wanatakiwa kuja fedha hizo zitatumikaje kwa kupata taarifa kutoka kwa viongozi wa Kijiji ambapo mtendaji wa Kijiji hicho ametoa taarifa ya mradi huo mbele ya wananchi.
Akitoa taarifa ya mradi mtendaji wa Kijiji Cha Mulahya Coelestin Barthazar amesema kuwa mradi huo wa ujenzi wa jengo la mama na mtoto Hadi Sasa umeghalimu jumla ya shilingi milioni 4,459,300 ambapo shilingi milioni 1,087,300 zimetolewa na wananchi huku milioni 1,582,000 waziri wa mambo ya ndani na mbunge wa Jimbo la Bukoba vijijini mh Jason Rweikiza akitoa milioni 1.
Aidha amesema kuwa Kijiji Cha Mulahya kinavyo vitongoji 6 kaya 680, nguvu kazi 708 watoto waendo clinik 453 huku jumla ya wananchi wote katika Kijiji Cha mulahya kata katerero wakiwa ni elfu 20404.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Mh.Murshid Ngeze amesema halmashauri kwa kushirikiana na ofisin ya mkurugenzi wametoa shilingi milioni 50 kwa ajili ya kumaliza ujenzi wa jengo la mama na mtoto lengo likiwa ni kuwasaidia wananchi kuondokana na kero hiyo ya kutembea umbali wa mda mrefu kwenda kituo Cha afya Cha kata Jirani.
Pia ameongeza na kusema kuwa kiwango Cha elimu kimeshuka hivyo na kuwataka wazazi kuwafuatilia watoto wao katika maendeleo ya mason yao Ili kuondokana na jambo hili la kushuka kwa kiwango Cha ufauru katika halmashauri hiyo.
Nao baadhi ya wananchi wameushukuru uongonzi wa halmashauri hiyo kwa kuwawezesha na kuwapatia fedha hiyo kwa ajili ya kumaliza ujenzi huo kwani walikuwa wakipitia wakati mgumu sana kwa kutembea umbali mrefu kufuata huduma.
Sambamba na hayo wameouomba uongonzi wa halmashauri hiyo kuwasaidia kumalizia ujenzi wachumba kimoja Cha darasa la chekechea kilichopo kitongoji Cha Lugoba kwa ajili ya kuwasaidia watoto wadogo.